December 21, 2012


PATA HII:

NI BAADA YA MHE.GODBLESS LEMA KUSHINDA RUFAA YAKE YA USHINDI WA UBUNGE WA ARUSHA MJINI LEO.........

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kwa Tiketi ya CHADEMA (aliekuwa amesimamishwa Ubunge),Mh. Godbress Lema akiwasalimia wanachamana na wafuasi wa Chama hicho waliokuwepo ndani ya Mahakama ya Rufaa,jijini Dar es Salaam leo.wakati alipofika kusikiliza Rufaa yake dhidi ya kesi ya Kupinga matokeo ya Uchaguzi dhidi yake iliyofunguliwa na Wanachana wa CCM jijini Arusha.Mh. Lema ameshinda Rufaa hiyo na kufanikiwa kurudishiwa nafasi yake ya Ubunge wa Jimbo la Arusha mjini.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Freeman Mbowe (katikati) akiwa sambamba na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,Godbress Lema (pili kulia) na Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassari wakiwa ndani ya Mahakama ya Rufaa,jijini Dar es Salaam leo wakati wa kusikiliza Rufaani ya kupinga matokeo ya Uchaguzi iliyokuwa ikimkabili Mbunge,Godbress leo ambaye ashinda Rufaa hiyo leo.
Wanachama na Wafuasi wa CHADEMA wakimshangilia Mbunge wao mara baada ya kushira Rufani ya kesi yake ya kupinga matokeo ya Uchaguzi jimbo la Arusha mjili iliyokuwa ikisikilizwa leo kwenye Mahakama ya Rufaa,jijini Dar es salaam.
 Wanachama na wakereketwa wakitembea kwa maandamano kuelekea kwenye ofisi za Chama zilizopo Kinondoni jijini Dar.
 Mwanamama huyu ambaye ni Mama ntilie nae hakutaka kuwa nyuma katika kushangilia ushindi wa Mbunge Mhe. Lema.
 Mhe. Lema akipokewa kwa pongezi kubwa kutoka kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA Mhe. Wilbrod Slaa.
Katibu Mkuu wa CHADEMA,Mhe. Wilbrod Slaa akizungumza na vyombo vya Habari baada ya Ushindi wa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,Mh. Godbress Lema.