DKT. SHEIN AONGOZA MKUTANO WA SABA WA BARAZA LA BIASHARA LA ZANZIBAR, (ZBC)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiendesha kikao cha Mkutano wa Saba wa Baraza la Biashara la Zanzibar, (ZBC) kilichofanyika katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar,(kushoto) Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko,Nassor Ahmed Mazrui,na katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abdulhamid Yahaya Mzee.
Baadhi ya waalikwa kutoka Taasisi walioshiriki katika Mkutano wa Saba wa Baraza la Biashara la Zanzibar, (ZBC) kilichofanyika katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar.
Rais mstaafu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara,Viwanda na Wakulima,(Chamber of Comance) Zanzibar,akichangia mada wakati wa Mkutano wa Saba wa Baraza la Biashara la Zanzibar, (ZBC) kilichofanyika katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar.
Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja, Vuai Mwinyi,akichangia mada iliyozungumzia Utalii wakati wa Mkutano wa Saba wa Baraza la Biashara la Zanzibar, (ZBC) ulichofanyika katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Mpendae,pia Mfanya Biashara Salum Turky,alipokuwa akichangia kuhusu suala la ujenzi wa viwanda vipya vitakavyo ondoa tatizo la Ajira kwa wananchi wakati wa Mkutano wa Saba wa Baraza la Biashara la Zanzibar, (ZBC) ulichofanyika katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Marium Hilali,(kushoto) wa kikundi cha Zaspo cha Kiembesamaki,wilaya ya Mahgaribi Unguja, wakati alipotembelea maonesho ya Bidhaa mbali mbali za Vikundi vya wajasiria mali yaliyofanyika leo katika mkutano wa Saba wa Baraza la Biashara katika viwanja vya Salama Bwawani
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Nassor Hamadi Omar, wa (ZOP) Zanzibar Orgave Prodiusears, cha Fuoni Unguja, wakati alipotembelea maonesho ya Bidhaa mbali mbali za Vikundi vya wajasiria mali yaliyofanyika katika mkutano wa Saba wa Baraza la Biashara katika viwanja vya Salama Bwawani
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Tatu Suleiman wa kikundi cha Zaidat Oil & Soap Spice,cha Chukwani Magharibi Unguja,(kushoto) alipokuwa akiangalia mafuta ya wakati alipotembelea maonesho ya Bidhaa mbali mbali za Vikundi vya wajasiria mali yaliyofanyika leo katika mkutano wa Saba wa Baraza la Biashara katika viwanja vya Salama Bwawani Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiangalia kitabu wakati alipotembelea Kikundi cha Moto Hand Craft, cha Pete Wilaya ya Kusini Unguja,ambacho kinazalisha nguo aina ya Batiki,maonesho ya vikundi mbali mbali vya Wajasiria mali yaliyofanyika katika mkutano wa Baraza la Biashara katika viwanja vya Salama Bwawani Zanzibar.
(Picha na Ramadhan Othman,Ikulu Zanzibar.)
WATANZANIA TUNAOMBWA TUOKOE MAISHA YA MTOTO HANIFA (MIAKA 5) KWA MICHANGO MBALI MBALI YA KUFANIKISHA MATIBABU YAKE
Mtoto Hanifa Salum Hassan mwenye umri wa miaka mitano anasumbuliwa na ugonjwa wa Saratani ya Damu (Leukemia) ambao umemfanya ashindwe kusimama na kutembea, anasumbuliwa na maumivu ya kichwa wakati wote, wakati mwingine hushindwa kupumua hivyo kulazimika kupumua kwa kutumia mashine pia hawezi kula analishwa kwa kutumia mirija na pia kila baada ya muda inabidi abadilishiwe damu.
MATIBABU
Matibabu ya mtoto Hanifa ni ya gharama kubwa sana. Ugonjwa wake haukujulikana alipopelekwa Hospitali ya taifa Muhimbili lakini alipopelekwa nchini India gharama za uchunguzi pekee zilikuwa dola 7,600 ambapo mtoto Hanifa aligundulika kuwa na ugonjwa wa Acute lymphoblastic Leukemia.
Matibabu yake yalipangwa yawe kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza ya matibabu iligharimu dola 10,000. Mwisho wa awamu ya kwanza zilihitajika dola 10,000 zingine ili aingie kwenye awamu ya pili ya matibabu lakini uwezo wa ndugu na jamaa ulikuwa ndio umeishia hapo hivyo matibabu ya mtoto Hanifa yalilazimika kukatishwa na Hanifa kurudishwa Tanzania.
Ripoti za madaktari India zilipelekwa Muhimbili ambapo matibabu ya mtoto Hanifa yalipangwa kugharimu Tsh. milioni 2 kwa mwezi.

Hakuna pesa za kumwezesha mtoto kuanza matibabu Muhimbili hivyo mtoto Hanifa amebaki nyumbani jijini Dar es Salaam akiwa kwenye hatari kubwa ya maambukizi mbalimbali ambayo yanaweza kuhatarisha maisha yake.
Hadi sasa ndugu na jamaa wanahaha kutafuta pesa za kumwezesha mtoto Hanifa kumalizia awamu mbili za matibabu yake nchini India kama ikiwezekana au ikishindikana basi aweze kuanza matibabu Muhimbili.
MICHANGO
Kwa watakaopenda kujitolea kuokoa maisha ya Mtoto Hanifa wanaombwa watoe michango yao kupitia akaunti hizi
Kwa walio Tanzania
Jokha Khamis Issa
Akaunti Namba: 041212000428
People Bank of Zanzibar
Kwa mawasiliano namba ya simu ni: +255 777 462587
Kwa walio nje ya Tanzania wanaweza kutuma michango yao kwa akaunti hii
Suleiman Maadini
Account Number: 15092968
Sort Code: 30-67-99
Bank: Lloyds TSB
Country: United Kingdom
Kwa mawasiliano na Bwana Maadini: +44 78 18674305
