January 09, 2013

 BUS LA BUNDA EXPRESS LAUWA ENEO LA MAGU MWANZA

Eneo la katikati ya Lugeye na Nyanguge Basi la abiria la 'Bunda express" lenye namba za usajili T 782 BKZ likitokea Musoma kuelekea jijini Mwanza muda wa saa mbili asubuhi hii limepata ajali mbaya kwenye eneo hilo.
Mazingira yanaonesha kuwa idadi kubwa ya watu wamejeruhiwa na hofu kubwa imetanda eneo la tukio kuhofia usalama wa hali za abiria waliomo ndani ya basi husika kwani basi limepinduka tairi zikielekea juu, limetumbukia kwenye majaruba ya mpunga, limepondeka vibaya upande mmoja, na tayari katika muda huu napita eneo la tukio miili ya watu wawili imeonekana ikizagaa nje ya basi kandokando ya barabara na mvua kubwa inaendelea kunyesha.
Hali ya uokoaji imeathiriwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha eneo hili ni wachache tu abiria wameweza kupewa miamvuli na watu walio kwenye magari yanayopita eneo hili ili wapate kujisitiri.
Chanzo cha ajali kinatajwa kuwa ni mwendo kasi wa busi hilo.
Watoto wakiwa na mama zao wanalia tu wakihitaji msaada, mvua ikiwanyeshea wakihofia usalama wao na mali zao. 
Mpaka tunaenda mitamboni idadi ya watu waliopoteza maisha ni wawili na (majina hayakuweza kupatikana maramoja) na 36 ni majeruhi
Watu 24 waliopata majeraha makubwa wamepelekwa hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza
Na majeruhi 12 wamepelekwa Hospitali ya Wilaya ya Magu. 
Hakuna pa kujisitiri kwa watoto hawa ambao walikuwa wakisubiri wazazi wao kuokolewa kutoka ndani ya basi hilo.
Ni uzuni kubwa 
Baadhi ya nyumba zilizo karibu na eneo la ajali nazo zimeathiriwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha eneo hili wilayani Magu.
Hali ya baadhi ya barabara za ndani zinazounganisha vijiji wilayani Magu zimefunikwa na maji
Barabara hali ya hewa na mazingira.
BLOGTz. inawapa pole wale wote waliopakumbwa na ajali hii mbaya.