September 30, 2012

MAHAFALI YA 4 YA F- IV EAGLE SEC BAGAMOYO





Shule ya Sekondari EAGLES ni Shule ya Bweni (Wavulana) iliyoko Wilayani Bagamoyo Mjini.
Shule ilianzishwa mwaka 2006 ikiwa na idadi ya wanafunzi 27 na hadi sasa shule ina idadi ya Wanafunzi 622 kwa Vidato vyote - KIDATO CHA I HADI VI.
Shule ilizinduliwa Rasmi na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo ( WAMA) ambaye ni Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Mama Salma Kikwete mnamo Tarehe 24, Oct. 2009.
Shule imejijenga katika Misingi ya kutoa Taaluma bora kwa vijana / wanafunzi ili kuwawezesha  kukabiliana na hali halisi ya maisha yao, kuwa mfano bora kwa shule za wavulana hapa nchini, kuongeza fursa kwa vijana hapa nchini kupata elimu iliyo bora,kuongeza nguvu kazi iliyoelimika hapa nchini nk..





Picha juu na chini: Sehemu ya wanafunzi Wahitimu Kidato cha Nne wakiwa katika pozi la picha katika eneo la shule hiyo kabla ya Mahafali yao kuanza.
Twende kazi......
Wahitimu wakicheza "Kwaito" kuingia katika viwanja vilivyoandaliwa kwa mahafali yao na wageni wote. 


Hapa Meza Kuu ikiwalaki wahitimu kwa kupiga makofi , vigeregere  nderemo na vifijo


Mkuu wa Shule  (Eagles Sec) akawakaribisha wageni waalikwa na kutambulisha rasmi meza kuu. 


Picha juu na chini: vijana wanafunzi wakiingiza igizo linalohusu mazingira ya adhabu zinzotolewa katika Taasisi za Elimu nchini na mapokeo yake kwa Jamii nzima. Vijana walisistiza na kusifu muendelezo wa kuwepo kwa adhabu hizo katika Taasisi mbalimbail za Elimu kwani bila adhabu, adabu haitaswihi.


                                               Kula hiyo....kamuonyeshe ..........


Sehemu ya wanafunzi wa Vidato mbalimbali wakionekana kunogewa na Maudhui ya Igizo hilo lililokonga nyoyo za waalikwa pia.


Vijana wakasoma Risala yao ya kuhitimu na kutoa shukurani zao za dhati kwa uongozi mzima wa shule hiyo kwa kuwapatia Elimu ambayo ndiyo msingi wa maendeleo kwao na jamii kwa ujumla.

Hapa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shule Mhe.Mama Generose Tabalo akapata fursa na kuzungumza na hadhara kubwa uliyohudhuria Mahafali hiyo. Katika hotuba yake Mhe. Mama Tabalo alibainisha mambo mengi na mazuri ambayo wanafunzi wanaopata fursa ya kusoma katika shule hiyo wanayapata.
Nguvu kazi:
Shule ina jumla ya walimu 40. Walimu wanne - 4 - wana Stashahada ya ualimu, walimu-33- wana shahada ya kwanza ya ualimu chuo kikuu, na walimu -3- wana Shahada ya pili.
Shule haina upungufu wa walimu
Kitaaluma:
  • Shule hii imekuwa na Taaluma ya kulidhisha pamoja na uchanga wake! Kwa matokeo ya Mitihani ya NECTA kwa Kidato cha Nne-IV-mwaka 2009 shule ilikuwa ya 21 kati ya shule 241 Kitaifa na ya kwanza -1-  Kimkoa kwa shule zenye watahiniwa chini ya 35. Miaka mingine : 2010 Eagles ikawa ya 54 kati ya Shule 3196 Kitaifa na 4 kati ya 91 Kimkoa kwa shule zenye watahiniwa zaidi ya 35.  Mwaka 2011 Eagles ikawa ya 43 kati ya shule 3801 Kitaifa na 3 kati ya 91 Kimkoa
Ni imani yetu kuwa taswira ya mafanikio haya mazuri kitaaluma itajionyesha pia katika matokeo ya mitihani ya mwaka huu na ijayo..  
Mkuu wa Mkoa Mstaafu ambaye ni Kamishna Mkuu wa Sensa nchini Mhe.Hajat Amina Mrisho(wa katikati mbele) alikuwa ni miongoni mwa wazazi waliohudhuria Mahafali haya. Katika picha anaonekana pamoja na wazazi wengine wakifuatilia kwa umakini moja ya maonyesho ya ngoma ya shule  ikiburudisha 

Kushoto ni Sehemu ya majego ya nyumba za walimu wa shule hiyo.
   
Kulia ni moja ya majengo ya shule hiyo. Hilo ni jengo la madarasa ya kidato cha tano na sita.

Mhe Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania (mwenye miwani katikati) alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa pia.



"Tumetokelezea.....!!" KITOY kulia akiwa na wahitimu wenzake katika pozi la picha

Mgeni Rasmi katika Mahafali ya nne ya Shule ya Eagles, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe.Hajat Mwantumu Mahiza akihutubia katika sherehe hizo.

Mgeni Rasmi akatunuku vyeti kwa wahitimu 
Isiaka Kibamba akiwa na zawadi zake baada ya kuwa mwanafunzi bora kitaaluma shuleni hapo.


Hapa Mgeni Rasmi akisisitiza jambo baada ya kubaini kuwa kijana mwanafunzi Isiaka Kibamba pichani juu ambaye alipata tuzo za vikombe saba (7), kwa kufanya vizuri zaidi katika masomo yake dhidi ya wanafunzi wenzake. 


Kitoy akitunukiwa cheti na zawadi ya kikombe cha chai chenye logo ya shule na picha yake kama kumbukumbu kwake.



Kitoy akiwa katika furaha kwa kulakiwa na wazazi wake punde baada ya kutunukiwa cheti.

Picha ya pamoja ya wahitimu, uongozi wa shule na mgeni rasmi ikapigwa. 

KARIBU EAGLES SEC SCHOOL BAGAMOYO.