October 16, 2012

IMTU NA KODI YA MAJENGO TSHs.100/= TU KWA MWAKA

Chuo Kikuu Cha Kimataifa Cha Tiba  na Teknolojia -IMTU- cha Mbezi Beach Jijini Dar Es Salaam kimekuwa kikilipa Tsh. 100/= tu kwa mwaka [ Shilingi za kitanzania mia moja tu kwa mwaka ]ikiwa ni  kodi/ada  ya pango la Majengo kinayoyatumia kwa ajili ya kuendeshea shughuli zake.
Chanzo chetu kimebaini kuwa IMTU ilisaini mkataba wa makubaliano hayo ya ada tangu tarehe 28 Agosti 1996 baina ya IMTU na Ndg. Rumisha Kimambo kwa niaba ya Shirika la Saruji Tanzania [Mpangishaji] na Ndg. Subba Rao kwa niaba ya Taasisi ya Vignan Educational Foundation -VEF- ya India [Mpangaji] inayomiliki kwa miaka 15 ambapo kod/ada ya jumla ilikuwa ni Tsh 1500/= tu kwa miaka 15.
Hata hivyo umiliki wa majengo hayo mwaka 2007 ulihamishiwa kwa Shirika la Maendeleo la Taifa -NDC- miaka minne kabla ya mkataba kufika kikomo. 
IMTU baada ya mmiliki kubadilishwa , iliomba kuongezewa mkataba wa miaka 25 zaidi kwa kulingania makubaliano ya mkataba wa awali [saruji] !
Hata hivyo baada ya mkataba wa awali kuisha Agosti 28 mwaka 2011, mmiliki mpya wa majengo hayo -NDC- alivunja mkataba wa awali na kuandaa mkataba mpya ambapo kwa mujibu wa mkataba huo mpya IMTU sasa inapaswa kulipa kodi/ada ya Tsh.73 Milioni tu[Shilingi za kitanzania milioni sabini na tatu tu] kwa mwezi kwa muda wa miaka mitano mitano tu na si Tsh 100 tena kwa miaka 15 wala 25 waliyokuwa wameomba kuongezewa.
IMTU haikukubaliana na masharti ya mkataba huo wa NDC[mmiliki/mpangishaji]  ambapo Mmiliki aliiomba IMTU kuondoka ili kutoa nafasi kwa mwekezaji mwingine anayeweza kukudhi masharti ya mkataba huo mpya.
Kutokana na tishio hilo la kutimuliwa IMTU katika harakati zake za kuinusuru bodi ya wadhamini wake, imekimbilia mahakama Kuu ya Ardhi ambako imefungua kesi dhidi ya NDC kupinga nia ya NDC !
Kesi hiyo Namba 210 ya mwaka 2012 ilifunguliwa Mahakamani hapo kupitia Wakili wa wadhamini hao wa IMTU mnamo Sept.22 mwaka huu.
Chanzo:
Mwanachi News.