October 18, 2012

Naibu jaji mkuu wa Kenya ajiuzulu




Aliyekuwa naibu jaji mkuu wa Kenya Nancy Baraza
Naibu jaji mkuu wa Kenya Nancy Baraza amejizulu baada ya jopo la majaji kutaka aachie ngazi kufutia madai ya kutishia maisha ya mlinzi mmoja kwa bunduki katika duka moja la kifahari Jijini Nairobi mapema mwaka huu.
Nancy Baraza alisema kuwa alihisi haki isingetendeka ikiwa engekata rufaa dhidi ya uamuzi wa jopo la majaji maalum waliosikiza kesi dhidi yake na kupeleka kesi yake katika mahakama ya juu zaidi nchini.Aidha ameelezea kuwa majaji wengine wawili katika mahakama hiyo walipendekeza kuwa jopo liundwe ili kuchunguza madai dhidi yake.Aliongeza kuwa jaji mkuu wa Kenya Willy Mutunga ambaye ni rais wa mahakama ya juu zaidi, alipitisha mapendekezo ya jopo hilo la majaji katika mahojiano kwenye televisheni na kwa hivyo asingetoa uamuzi wa haki kwenye kesi yake ya rufaa.Jopo la majaji saba likiongozwa na aliyekuwa jaji mkuu wa Tanzania, Augustino Ramadhani, ilimpata Baraza na hatia ya kutishia maisha ya mlinzi Rebecca Kerubo, katika duka la kifahari la Village Market alipotaka kupekua kibeti chake kabla ya kuingia kwenye duka hilo.Ulinzi nchini Kenya umedhibitiwa sana hasa baada ya jeshi la Kenya kwenda Somalia kupambana na Al Shabaab. Na kila sehemu ya maduka walinzi hupekua mizigo ya watu kama tahadhari tu ya kuhakikisha usalama wa watu.