October 19, 2012

Rais wa Malawi Joyce Banda ametaka AU kuingilia kati mzozo Tanzania na Malawi.

 Rais Joyce Banda wa Malawi amesema Malawi inajiondoa katika mazungumzo ya mvutano wa kuhusu wapi hasa mpaka halisi ulipo baina ya Tanzania na Malawi na sasa nchi yake inafikiria kuupeleka mzozo huo katika mahakama ya kimataifa.
Rais wa Malawi Joyce Banda
Ziwa Malawi, au Nyasa ni moja kati ya maziwa makubwa ya Afrika na ni la nane kwa ukubwa duniani. Ziwa nyasa linapakana na nchi za Msumbiji, Malawi na Tanzania.
Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda alikuwepo London na amezungumza na Salim Kikeke kuhusu suala hilo.