MAONYESHO YA VIFAA VYA UJENZI NA SAMANI ZA NDANI YAFUNGWA RASMI JIJINI DAR
Afisa uhusiano wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi. Roida Andusamile (wa pili kushoto) akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi. Jacqueline Mneney Maleko (wa pili kulia) kugawa vyeti kwa washiriki sambambamba na kufunga Maonyesho ya Vifaa vya Ujenzi na Samani za ndani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Tanzania Building and Home Improvement EXPO 2012 Bw. Zakaria Malcom ambao ndio waandaaji wa maonesho hayo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi. Jacqueline Mneney Maleko akizungumza na washiriki wa maonyesho hayo kabla ya kugawa vyeti na kisha kuyafunga rasmi ambapo amewataka washiriki kuwasilisha Profile za makampuni yao katika mamlaka husika pamoja na kushiriki maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Saba saba yatakayofanyika mwakani.
Pia amewataka washiriki kujijengea utamaduni wa kuzunguka katika maduka mbalimbali yanayouza vifaa vya ujenzi na samani za ndani kuangalia ubora wa bidhaa ili kugundua iwapo zinachakachuliwa na wafanyabiashara wa kigeni na kuwaasa kuongeza ubora wa bidhaa wanazozitengeneza kuwa na kiwango cha kimataifa ili kwa kushirikiana na mamlaka yake waweze kupata soko nje ya nchi.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Alredha Lighting wanaopatikana Mkabala na Shoppers Plaza Mikocheni Bw. Riyaz Jetha akipokea cheti cha ushiriki bora katika maonyesho hayo kutoka kwa Bi. Jacqueline Mneney Maleko.
Pichani Juu na Chini baadhi ya washiriki wa maonyesho ya Vifaa vya Ujenzi na Samani za ndani wakipokea vyeti vyao vya ushiriki bora.
Mwakilishi wa Kampuni ya Masoko na Matangazo ya Advent Promotions Nassara Peter akipokea cheti.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi. Jacqueline Mneney Maleko akibadilishana mawazo na baadhi ya washiriki wa maoneysho hayo. Kulia ni Meneja Mauzo Afrika Mashariki wa Kampuni ya Alredha Lighting Bw. Mohammed Mustafa na Katikati ni Mwakilishi wa Kampuni ya Masoko na Matangazo ya Advent Promotions Nassara Peter.
Meneja Mauzo Afrika Mashariki wa Kampuni ya Alredha Lighting Bw. Mohammed Mustafa akionyesha uimara wa moja ya bidhaa zinazopatikana katika duka la Alredha Lighting.
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya washiriki wa Maonyesho ya Vifaa vya Ujenzi na Samani za Ndani yaliyokuwa yakifanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam na kufungwa jana. Maonyesho hayo yaliyodumu kwa siku tatu yaliandaliwa na Kampuni ya Tanzania Building and Home Improvement EXPO 2012.