November 18, 2012


"Matatu" yashambuliwa eneo la Eastleigh jijini Nairobi

Watu 5 wamesadikiwa kupoteza maisha katika mripuko huo uliotekea kwenye gari dogo maarufu "matatu" jijini Nairobi.
Mji wa Nairobi
Taarifa za awali zinaonesha mripuko huo ulisababishwa na shambulio la guruneti.
Shambulio hilo limetokea karibu na kanisa katika mtaa wa Eastleigh ambao una wakaazi wengi wa Kisomali.
Kumekuwepo na vitendo vya  mashambulio ya mara kwa mara jijini Nairobi tangu jeshi la Kenya kuingia nchini Somalia ili kudumisha usalama tangu mwaka jana.