Mashabiki wa soka wakiingia uwanjani Taifa kushuhudia game
Upande wa jukwaa la shabiki wa Yanga Africa ulinona na kupambwa na bendera.
TV ya matokeo ilikuwa kama ilivyo pichani kabla ya mpira kuanza
Soka likaanza .
Siku hii nilikaa na mashabiki upande fulani nikisikiliza na kufuatilia simulizi rukuki kuhusu mpira wa kibongo. Nashauri kama wewe pia ni mdau na shabiki mzuri wa soka kwa ujumla, tengeneza ratiba ya uingia ground na kufuatilia mwenyewe kile unachokipenda katika soka.
Ghafla dakika ya 9 tu ya mchezo Yanga ikaandika bao la kwanza na kuwainua mashabiki wake jukwaani kwa shangwe na vigeregere....
Baada ya goli hili kushangiliwa kwa vifijo na nderemo, misemo na sifa rukuki toka kwa mashabiki ziliendelea kuwamiminikia wachezaji wa Yanga kutokana na kuzisikia kutoka upande huo nilikokuwa nimeketi pia. Hadi mapumziko ubao ulisomeka 1bila.
Ubao ukabadirika na kuonyesha nafasi ya ushindi mnono kwa yanga dhidi ya Azam
Mtoto wangu wa kike Husna Yakubu akishangilia kwa kuonyesha vidole viwili juu akiashilia kushangilia kwa furaha pia. Kushoto kwake ni kaka yake, Hussein Yakubu
Mwisho