November 15, 2012

TUOKOE MAISHA YA MTOTO HUYU.

Shilingi milioni sita zinahitajika kwa ajili ya matibabu ya mtoto Selemani Said mwaka mmoja
 ambaye anajisaidia haja kubwa kupitia utumbo mkubwa huku ukiwa nje ya tumbo lake
Akizungumza na wandishi wa habari 
katika Ukumbi wa Idara ya 
Habari (Maelezo),jijini 
Dar es Salaam leo, mama wa mtoto 
huyo, Veronika Laurent ambaye ni 
mkazi wa Bunju, alisema mtoto huyo
alizaliwa huku akiwa na sehemu ya
kutolea haja kubwa lakini cha 
kushangaza, haja kubwa ilikuwa 
ikitokea mdomoni.

Alisema msaada wa fedha hizo 
utasaidia katika kumfanyia 
operesheni mtoto huyo ambaye
 kwa sasa anaishi akiwa katika 
mateso makubwa.

Veronika alisema hivi sasa yeye pamoja na mwanaye huyo wanaishi maisha ya kubahatisha baada ya
 baba wa mtotohuyo kuitelekeza familia hiyo kutokana na hali ya ugonjwa wa mtoto huyo.

“Mimi ninachokiomba ni msaada wa fedha ili niweze kumpeleka kwenye matibabu kwani sina msaada 
wowote,ukichukulia wazazi wangu kufariki na hivi sasa naishi 
kwenye nyumba ya  mwenyekiti wa Mtaa wa Bunju Wilayani Kinondoni Jijini 
baada ya kushindwa kupangisha chumba kwani sina kazi yeyote”alisema mama huyo.

Aidha, alisema hadi utumbo wa mtoto huyo kutoka nje, ni baada ya kufanyiwa operesheni
 katika hospitali ya
 Taifa ya Muhimbili ambapo hata alipompeleka tena kwa ajili ya matibabu alikosa ushirikiano 
kutoka kwa
madaktari
 na wahudumu wengine.
Alisema kwa yeyote ambaye yuko tayari kumsaidia anaweza wasiliana naye kwa kupiga simu 
namba
: o715 83 77 00, au namba ya mwenyekiti  wa mtaa 0656780236.

Veronika ni mzaliwa wa Mkoa wa Kilimanjaro eneo la Kijiji cha Uru,Moshi ambye alimzaa mtoto 
huyo na 
mwanamme
 aliyemtaja kwa jina la Abdalah Said, kabilake mmakonde mfanyabiashara wa viatu Ubungo.