HALMASHAURI ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma imepiga marufuku shule za msingi zenye upungufu wa vyumba vya madarasa kutumia vibanda vilivyojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi kama vyumba vya madarasa.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Steven Nana katika mahojiano na mwandishi wa makala haya alisema katika mkutano wa Baraza la madiwani uliofanyika mwezi Juni mwaka huu walipendekeza shule zote ambazo zinatumia madarasa ya vibanda vilivyojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi kuvibomoa badala yake kujenga madarasa kwa kwa kutumia tofali za kuchoma.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Steven Nana katika mahojiano na mwandishi wa makala haya alisema katika mkutano wa Baraza la madiwani uliofanyika mwezi Juni mwaka huu walipendekeza shule zote ambazo zinatumia madarasa ya vibanda vilivyojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi kuvibomoa badala yake kujenga madarasa kwa kwa kutumia tofali za kuchoma.
“Hadi sasa madiwani katika kata zenye shule ambazo wanafunzi wanasomea vibanda vya nyasi wameitikio wito vibanda vimebomolewa na kujenga vyumba kwa tofali za kuchoma kwa mfano kata za Mgombasi, Luchiri na Msindo,kata ambayo bado hawajatekeleza ni uzembe wa usimamizi wa diwani husika, vibanda vya nyasi sio mazingira rafiki kwa kusomea wakati wa mvua vinavuja na kuathiri taaluma”, alisisitiza.
Vibanda vya nyasi bado vinatumika katika shule ya msingi Selous, hapa ni wanafunzi wa darasa la tano wakisoma katika mazingira duni
Hata hivyo alisema wananchi waliamua kujenga vibanda vya nyasi kwa lengo la kukabiliana na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa ambapo alisema serikali ilitoa masharti magumu kwa wananchi kwa kuwataka wajenge vyumba vya madarasa kwa kutumia kokoto kwenye msingi na kujenga kwa theluji badala ya udongo jambo ambalo wananchi walishindwa kumudu gharama za ujenzi.
Kutokana na hali hiyo mwenyekiti huyo anasema walipendekeza wananchi kujenga vyumba vya madarasa kwa udongo na tofali za kuchoma ambapo serikali iliahidi kuchangia vifaa vya kiwandani ambapo hadi sasa tayari wananchi wamefyatua tofali na fedha zitakapopatikana wanapewa ili kukamilisha ujenzi.
“Halmashauri yangu inakabiliwa na upungufu mkubwa wa fedha katika mwaka wa fedha wa 2012/2013 ilitengewa shilingi bilioni 16 lakini hadi kufikia mwezi huu Desemba ni asilimia 14 tu ya fedha ndiyo imefika kutoka TAMISEMI, fedha ikipatikana tutazipeleka katika shule kwa ajili ya kukamilisha ujenzi”, alisema
Uchunguzi ambao umefanywa katika shule tatu za msingi kata ya Rwinga wilayani Namtumbo ambazo ni Rwinga, Kidugalo na Mkapa umebaini shule hizo zimefyatua tofali 80,000 kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu.