December 19, 2012


JOSEPHAT CHARO ARITHI MIKOBA YA OTHMAN MIRAJI IDHAA YA KISWAHILI YA DEUTSCHE WELLE 

Mtangazaji Mwandamizi wa Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani (Deutsche Welle), Josephat Charo (kulia) leo hii amekabidhiwa rasmi mikoba ya kuwa Mhariri Mwandamizi wa Idhaa hiyo,iliyoachwa na Othman Miraji aliyestaafu hivi karibuni. Kushoto ni Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili,Andrea Schmidt mara baada ya kutangaza wadhfa huo katika hafla maalum iliyofanyika mjini Bonn,Ujerumani.
Pichani toka kushoto ni Mhariri Mwandamizi wa Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani (Deutsche Welle),Josephat Charo, Abdul Mtullya, Sylivia Mwehozi na Bruce Amani wakati wa hafla maalu,iliyofanyika leo mjini Bonn,Ujerumani.
Kutoka kushoto ni Josephat Charo, Nina Markgraf na Sudi Mnette wakiwa pamoja kwenye hafla hiyo.
Mdau Sudi Mnette akiwa na zawadi ya chrismas na mwaka mpya ya kitabu ambacho alipewa kila mfanyakazi wa Dw na Mkuu wa Idhaa Andrea Schmidt.
wafanyakazi Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani (Deutsche Welle) wakifurahi pamoja baada mkuu wa Idhaa hiyo Andrea Schmidt kumtangaza Josephat Charo kuwa ni miongoni mwa wasaidizi wake wa karibu