Mapigano mapya MtoTana nchini Kenya.
Ni mapigano ya kikabila, wakulima na wafugaji.
Watu 39 wauawa hadin sasa..
Ramani ya Kenya
Takribani watu 39 wameuawa na wengi kujeruhiwa katika mapigano yaliyozuka upya katika eneo la MtoTana nchini Kenya baada ya wavamizi wasiojulikana kushambulia kijiji cha Kipao alfajiri ya leo.
Polisi wamethibitisha hayo na kusema huenda idadi hiyo ikaongezeka.
Shambulio hilo linadaiwa kufanywa na watu kutoka jamii ya Pokomo katika kijiji cha Kipao dhidi ya watu wa Kabila la Ormo.
Nyumba kadhaa zimeripotiwa kuteketezwa na watu kadhaa kujeruhiwa kwa kukatwa kwa mapanga.
Mapema mwezi wa Agosti na Septemba, Eneo hilo la Mto Tana lililopo pwani ya Kenya lilikumbwa na mapigano ya kikabila yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu mia moja, wakiwemo maafisa kadhaa wa Polisi.
Idara ya polisi imesema watu kutoka jamii hizo mbili walipoteza maisha yao na wengine kujeruhiwa wakiwemo watoto na wanawake.
Haki za malisho
Nyumba iliyochomwa huko Mto tana
Wakaazi katika vijiji kadhaa eneo hilo wamekimbia makwao wakihofia mashambulio ya kulipiza kisasi.
Shirika la msalaba mwekundu limesema takribani watu 30 wameuawa na wengine 30 kujeruhiwa vibaya, akiwemo mtoto wa umri wa mwaka mmoja.
Aidha shirika hilo linasema nyumba 40 ilichomwa na wavamizi hao.
Maafisa wa shirika hilo la msalaba mwekundu wanaendelea na msako katika eneo hilo kuwatafuta miili zaidi.
Maafisa zaidi wa polisi na maafisa wa kutoa misaada ya dharura wamepelekwa katika eneo hilo kwa ndege ili hali wale waliojeruhiwa wamesafirishwa hadi hospitali kuu ya mkuu mjini Mombasa.
Mwezi Agosti mwaka huu, jamii hizo mbili zilizozana baada ya wakulima kutoka kwa jamii ya Ormo kupeleka mifugo wao katika ardhi inayodaiwa kumilikiwa na watu wa jamii ya Pokomo.
Polisi wamekuwa katika eneo hilo kujaribu kuwapokonya silaha makundi hayo mawili.
Wakaazi wa eneo hilo wanasema uhasama kati ya jamii hizo mbili umekuwa ukitokota katika siku za hivi karibu