NI BAADA YA UTAFITI WAKE KUKAMILIKA.
Na Yakubu Mkaka
Mamlaka ya mawasiliano chini iko mbioni kuzifungia huduma / kuzizima simu zote zitakazogundulika kuwa zimeingizwa nchini zikiwa feki.
Hatua hii ya kimaendeleo tayari imeshafikiwa na nchi nyingi zikiwemo jirani zetu Kenya na Uganda.
Kwa Tanzania inaaminika kuwa zaidi ya wakazi milioni 27 yaani asilimia 60% ya wananchi wote, wanamiliki simu za mikononi. Wingi huu si haba kwani unachangiwa na umuhimu mkubwa uliopo katika kukuza mawasiliano na kurahisisha huduma za kimaendeleo za kila siku.
Ikumbukwe kuwa kwa sasa simu ni mbadala wa huduma za kibenki na hurahisisha miamala ya kifedha kwa haraka zaidi na tangu kutambulishwa kwa huduma hizi za kifedha katika simu, tathmini inaonyesha kuwepo kwa wepesi wa mzunguko wa fedha baina ya watu wa mijini na vijijini na jamii kwa ujumla.