TDL YAZINDUA KINYWAJI KIPYA CHA ZANZI CREAM LIQUEUR JIJINI DAR LEO
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL), Ndg David Mgwassa akitambulisha rasmi kinywaji hicho kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kinywaji kipya kinachoitwa ZANZI (kinachoonekana pichani).
Hafla hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL),Joseph Chibehe akitoa ufafanuzi wa Kinywaji hicho kipya aina ya ZANZI ambacho kinapatikana katika ujazo wa 750ml na katika Pakiti zenye ujazo wa 100ml ambacho kitakuwa kikipatikana nchi nzima.Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya TDL,David Mgwassa na kulia ni Meneja Usafirishaji wa TDL,Bavon Ndumbati.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL),David Mgwassa (katikati),Meneja Masoko wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL),Joseph Chibehe na Meneja Usafirishaji wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL),Bavon Ndumbati wote kwa pamoja wakigonganisha glass kuashiria uzinduzi rasmi wa kinywaji hicho uliofanyika leo kwenye hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam