Waandamanaji waizingira Ikulu ya Misri
Maelfu ya wapinzani wa rais wa Misri,Mohamed Morsi, wameapa kuendelea na maandamano yao nje ya ikulu ya rais mjini Cairo.
Baadhi wameweka mahema nje ya ikulu na sasa wanuzunguka ukuta wa ikulu hiyo.
Taarifa zinazohusiana
Siku ya Jumanne , maelfu ya waandamanaji walivamia ikulu wakipinga rasimu ya katiba iliyozua utata mkubwa pamoja na kupinga sheria inayomlimbikizia mamlaka makuu Rais Morsi.
Wakati mmoja polisi walifyatua gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji hao ambao walikuwa wamevuka ukuta wa seng'enge.
Vikosi vya usalama vilitoa taarifa vikisema kuwa rais Morsi ameondoka katika ikulu hiyo na ameomba utulivu.
Waandamanaji hao wanapinga hatua ya rais kujilimbikizia madaraka mapya na kusababisha kuundwa kwa rasimu ya Katiba.