Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hes
abu za Serikali Bw. Ludovick Utouh (kushoto) akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ukumbi wa mikutano wa Tume hiyo jijini Dar es Salaam (Jumamosi, Januari 19, 2013). Bw. Utouh alikutana na Wajumbe wa Tume hiyo kutoa maoni ya taasisi yake kuhusu Katiba Mpya.
Waziri Mstaafu na Mwanasiaisa Mkongwe nchini, Mzee. George Kahama (kushoto) akizungumza katika mkutano na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo katika ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam (jumamosi, januari 19, 2013) na kutoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya. Katikati ni Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba na Makamu Mwenyekiti, Jaji mkuu mstaafu Augustino Ramadhani