NELSON MANDELA HAJAMBO
Serikali ya Afrika Kusini inasema rais wa zamani wa nchi hiyo, Nelson Mandela, hajambo baada ya ugonjwa wa mapafu na upasuaji wa kutoa mawe kwenye apendex
Alikuwa hospitali kwa majuma kadha mwezi wa Disemba.
Taarifa rasmi iliwanukuu madaktari waliomtibu wakisema kuwa Mzee Mandela, mwenye umri wa miaka 94, amepata nafuu na afya yake inazidi kutengemaa.
Rais huyo Mstaafu amebaki nyumbani kwake mjini Johannesburg tangu alipotoka hospitali siku 11 zilizopita.