March 19, 2013

BAADHI YA MATUKIO YA ZIARA YANGU KANDA YA ZIWA FEB- MARCH,2013

 Meli ya MV Victoria inayofanya safari zake kanda ya ziwa Mwanza To Bukoba & vise versa ikiwa katika bandari ya Mwanza (North Port) ikipakiwa mizigo nyakati za mchana tayari kwa kawaida ya safari zake.
Ikumbukwe meli hii ina zaidi ya miaka 25 ikihudumu katika Ziwa Victoria.
 Picha juu na chini nashuhudia live ugomvi baida ya binti na kijana, kama picha zinavyoonekana binti akimng'ang'ania kijana ambapo ushuhuda usiorasmi iiliaminika kijana alitaka kupanda basi nililokuwa nimepanda kutoka chato kuelekea mwanza na kumuacha solemba binti ! ingawa mchoro ulivurugika baada ya binti kumkimbilia kijana ambaye tayari alikuwa anapanda basi na kuanza kumshusha kwa hasira na kumshushua kwa kitendo cha kuondoka kwa kumtoroka ambapo siku hiyo ilikuwa ni siku ya WAPENDANAO !!!!!!!! yaani tarehe 14-02-2013......kama unavyoona mavazi ya wapendanao hao...


 Katika picha juu na chini shuhudia ndege hawa wakifurahia kuwa katika ufukwe wa ziwa Victoria asubuhi na mapema.

 Hii ni Bandari ya Nansio Wilayani Ukerewe ingawa picha ilipigwa wakati wa ukinzani wa mwanga wa jua !!
 Moja ya fukwe za Ziwa Victoria. Kumbuka Ziwa hili sifa yake kubwa halina mchanga katika kina chake na inasadikika kina cha ziwa hili kimejaa tope zito ambalo mara nyingine halifai kwa kuokoa vyombo vya majini vinavyozama katika maji marefu ya Ziwa hili.!!
 Hapa kabla ya kuvuka napata fursa ya kupiga picha ya kumbukumbu ya kivuko hiki cha Kisorya nikitokea jimbo la mwibara bunda mkoani Mara kuelekea ng'ambo ya pili yaana Ngoma - Nansio Ukerewe.
 Baada ya Ziara yangu Kisiwani Ukerewe, iliyosheheni matukio kemkem; sasa narudi na Meli ya Mv Nyehunge ya Binafsi, na kushuhudia andishi kubwa la balimi extra lager katika soko maarufu kanda ya Ziwa, la  Mwaloni.

Kando ya soko la Mwaloni naona Meli Binafsi zikiwa zimepaki kwa muda zikisubiri kufanya ziara za hapa na pale ziwani.
Usikose mwendelezo wa matukio lukuki toka kanda ya ziwa.