Kitabu hiki kinahusu Vita vya Biafra vilivyodumu kwa muda wa miaka mitatu nchini Nigeria. Chinua Achebe alihudumu kama Balozi wa kimila katika eneo zima la Biafra, pale lilipojaribu kujitenga kutoka Nigeria mwaka 1967.Kitabu hicho kiliandikwa mwaka 1958. Kimetafsiriwa kwa zaidi ya lugha 50 na kinatilia mkazo tamaduni za jamii ya Waigbo zinavyogongana na maisha ya kizungu.Chinua Achebe ni mmoja wa waandishi wa vitabu mashuhuri na mkongwe zaidi barani Afrika ambaye kitabu chake cha kwanza kijulikanacho kama "things Fall Apart" kimeuza nakala milioni 10 kufikia hivi sasa.
Mwandishi huyo wa kitabu 'Birth pangs' ambaye ameshinda tuzo nyingi, na mpaka sasa ana umri wa miaka 81. Hadi leomwandishi huyu maarufu ameandika zaidi ya vitabu 20, vingi vikiwakosoa vikali wanasiasa na watawala wa taifa hilo.
Chinua Achebe kwa sasa anaishi nchini Marekani kufuatia ajali ya barabarani mwaka 1990. Hata hivyo hajagusia ghasia za mauaji katika Vita vya Biafra, ambavyo vilianza akiwa na familia yake changa. Ni mahala padogo sana anagusia vita hivyo katika mashauri yake.
Zaidi ya watu milioni moja waliuawa katika vita hivyo kutokana na mapigano na ukosefu wa chakula. Picha za watoto waliokonda kutokana na njaa katika magazeti ndizo zilizokuwa ishara ya vita vya Biafra.
Vitabu vya Chinua Achebe, hasa kile cha Things Fall Apart kimetumiwa katika fasihi ya Kiingereza kote katika Vyuo Vikuu na shule za upili katika Bara la Afrika na kwingineko.