September 26, 2012

MAMA ANNE MAKINDA KATIKA MAHAFALI BABRO JONSON SEC


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Anne Makinda leo Tarehe 25 Sept. 2012, amehudhulia mahafali ya kidato cha Nne na Tano yaliyofanyika katika viwanja vya shule hiyo. Akahutubia na kisha kuonyesha juu na kuinadi picha ya mchoro wa ramani ya Afrika kwa ajili ya kununuliwa.

Sehemu ya wageni waalikwa(meza kuu) katika pozi


Mheshimiwa Balozi Rupia akitoa neno la shukurani kwa Mgeni Rasmi na waalikwa wote katika mahafali hiyo.



Mgeni Rasmi akiwa katika picha na wanafunzi wa vidato tofauti tofauti wa shule hiyo baada ya kumkabidhi ua alilishikilia.

Kisha Mgeni Rasmi akapelekwa kuzindua Jengo la bwalo la chakula (Dinning Hall)

Mhe. Mgeni Rasmi Mama Anne Makinda akizindua Rasmi Jengo la bwalo la chakula la shule hiyo.
Mhe.Balozi wa Seeden Nchini akipikea pongezi za shukurani kutoka kwa Mhe.Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka punde baada ya Mgeni Rasmi Spika wa Bunge (Mama Makinda pichani katikati) kuzindua Rasmi Jengo la bwalo la chakula. Kushoto mwenye miwani ni Mkuu wa Shule hiyo.





                                         Jengo la Bwalo lililozinduliwa

                         Chini katika picha ni sehemu ya majengo mengine ya shule


Kamakawaida ujasiliamali huu wa picha za papo kwa papo ukaoneka kuchukua nafasi yake japo wauzaji wanadai wateja wamepungua sana kwa sasa kwani karibu asilimia zaidi ya 70 ya wateja wao wanamiliki ving'amuzi vyao vya picha!!!

Hapa kikundi cha ngoma kutoka Lugu Wilayani Karagwe Mkaoni Kagera kikiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Profesa Tibaijuka jioni baada ya shughuli za sherehe .