September 19, 2012

RAIS KIKWETE AFANYA ZIARA RASMI NCHINI KENYA

 Rais Kikwete afanya ziara rasmi ya kiserikali ya siku tatu nchini Kenya

Mhe. Rais Jakaya Kikwete na ujumbe wake ktoka Tanzania wakiwasili na kulakiwa na mwenyeji wao Mhe.Mwai E. Kibaki katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya Sept.11.2012.
Rais Kikwete na ujumbe wake wako katika  ziara ya kiserikali kwa siku tatu nchini humo.

 Rais Jakaya Kikwete akikata utepe kufungua rasmi jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta nchini Kenya. Kulia kwake ni Waziri wa Elimi ya Juu nchini Kenya, na kushoto kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kenyatta ,Profesa Olive Mugendi.

 Rais Jakaya Kikwete akihutubia hadhara na kufungua rasmi jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta nchini Kenya.

Waheshimiwa Marais Jakaya Kikwete na mwenyeji wake Mwai E. Kibaki pamoja na wajumbe kutoka nchi zote mbili(Tanzania na Kenya) wakiwa katika picha ya pamoja nje ya jengo la Ikulu,Jijini Nairobi