September 19, 2012

UZINDUZI WA BARABARA (DARTS) JIJINI DAR



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Jakaya Kikwete akizindua Rasmi Ujenzi wa Barabara  ya Mabasi yaendayo Kasi Jijini Dar Es Salaam (DARTS). Mradi huu unadhaminiwa na Benki Ya Dunia na mpaka kukamilika kwake utagarimu zaidi ya dola millioni 240. Uzinduzi huo umefanyika leo Tarehe Sep 19.2012 eneo la Viwanja vya Jangwani Jijini Dar.

Mtendaji Mkuu wa Mradi huo (DARTS) akitoa maelezo mafupi ya utekelezaji wa Mradi huo kwa Mhe Rais Kikwete. Hadi sasa ujenzi wa barabara hiyo unaendelea vizuri.

Mhe.Rais Dkt Jakaya Kikwete alipata fursa ya kukagua baadhi ya vifaa vinavyofanikisha ujenzi wa mradi huo kama anavyoonekena ndani ya chombo katika picha hii.