October 19, 2012


MAGARI YA SERIKALI YANAYOTUMIA NAMBA BINAFSI KUDHIBITIWAWaziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiteta jambo na Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Kamanda  Mpinga  Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (waliokaa mbele wapili kushoto) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kusisitiza  utaratibu wa usajili wa magari ya Umma unafuatwa na kutafanyika zoezi rasmi la kurejesha usajili wa magari yote.Serikali imetoa muda hadi kufikia Novemba 15,2012 magari ya Umma yaliyo na namba  za kiraia, yarejeshwe namba stahiki za magari ya Umma .  Baada ya hapo Operesheni hiyo iitakamata magari, pikipiki, bajaj na mitambo ya umma,Vilevle kutakuwa na aina ya namba za usajili zitakazotumika kama ST, PT, MT,JW, DFP, CW, SM na ,SU.Hadi sasa serikali imesajili vyombo vya moto,123,431 yakiwemo magari,,pikipiki,bajaj na mitambo ya umma (pichani anaefuatia mwenye sare za polisi) ni Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani katika jeshi la Polisi  nchini Kamanda James Mpinga). (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).