Polisi wa Doria wakipita katika mitaa iliyokuwa na vurugu katika eneo la darajani mjini Zanzibar ambako vurugu kubwa zimetokea na kusababisha kuuawa kwa kuchinjwa Polisi mmoja aliyetambulika kwa jina la Said Abdulrahman na wafuasi wa kundi la uhamsho linaloongozwa na Sheikh Farid ambaye amepotea katika mazingira ya kutatanisha. Hata hivyo Jeshi la Polisi mjini Zanzibar limekanusha kumshikilia kiongozi huyo na halijui mahali halipo.
Baadhi ya mali zilizoharibiwa katika vurugu hizo
Barabara katika mji wa Zanzibar zikiwa zimefungwa kwa mawe na kusababisha hadha kwa watumiaji pamoja na kufungwa maduka pamoja na biashara mbalimbali