October 19, 2012

MAPAMBANO YA DOLA NA WAANDAMANAJI JIJINI DAR ES SALAAM LEO


 Muumini wa dini ya Kiislamu akitoa shahada kwa mola wake na kusema nipo tayari kufa kwa ajili ya kutetea dini ya Allah, baada kukamatwa na Askari wa Kikosi cha Kutulia Ghasia katika viunga vya Ikulu leo. 
 Safari ya kuelekea Kituo Kikuu ilianza
Askari wa Kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU) wakijiandaa kumwingiza katika gari muumini wa Kiislamu aliyekamatwa katika maeneo ya Ikulu 
 Barabara ya kuingia katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi zikiwa zimefungwa na Askari Polisi kufuatia vurugu zilizotokea leo
Polisi wakifanya doria kwa kutumia pikipiki
 Mitaa ya Kariakoo na viunga vyake ikiwa imeimarishwa na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika mitaa ya Kariakoo leo
 Ulinzi uliimarishwa na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika mitaa ya Kariakoo leo
 Wanajeshi wakivinjari katika mitaa ya Kariakoo leo
 Askari wa jiji wakishiriki kikamilifu katika zoezi la kuwakamata watu waliokuwa wamekusanyika kwa nia ya kutaka kuandamana katika eneo la Kariakoo
Dar es Salaam, Tanzania