October 27, 2012

Mambo ya Zawadi za Kimila na Tamaduni Kutoka Harusini Leo

                 Zawadi ya kimila [kanzu] ikiandaliwa na Baba kwa mtoto wake..
 Mtoto[bwana harusi] akivaa vazi la kanzu baada ya kulipokea ikiwa ni  zawadi ya kimila  toka kwa baba yake.Zawadi hiyo na zinginezo za kimila hutolewa na wazazi ili kudumisha mila na tamaduni za kabila la Wahaya. Kabila la Wahaya asili yake ni Mkoa wa Kagera hapa nchini na ni Kabila linalosifika kwa sifa nyingi ikiwemo ya kufuta ujinga katika Familia kwa kiwango cha Elimu ya juu na 'Professionalism'...
 Kisha baba akamkabidhi mkuki ikiwa ni ishara ya kumkabidhi kijana [bwana harusi] siraha ya kuilinda nyumba yake mpya anayoenda kuianzisha na mkewe.
Kijana [bwana harusi] anapokea maneno machache ya kumhusia juu ya kuishi vyema na kudumu katika ndoa yake na mwenziwake aliyempata kwa maisha ya kufa na kuzikana. Bibi harusi katikati akionekana katika tabasamu la furaha ya kipekee ..
                                          Sehemu ya Keki yao ya Upendo
                         HAKIKA ILIKUWA NI HARUSI YA KUFANA SANA..........

                                            Picha Na : +255  714  422 177