October 26, 2012

POLISI YAWABAINI WALIOMUUA KAMANDA BARLOW


Majina ya watu watano  wanaotuhumiwa kuhusika moja kwa moja na kifo cha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Leberatus Barlow yametajwa rasmi leo jijini Mwanza.

Kabla ya hapo DCI Manumba alitoa taarifa juu ya uchunguzi uliofanywa na kikosi chake na kupelekea kunaswa wahusika hao ambaao ni; Muganyizi Michael Peter (36) ambaye inatajwa kuwa ndiye aliyemuua Barlow,Chacha Waitare Mwita (50)Magige Mwita Marwa (48),  Buganzi Edward Kusuta pamoja na Bhoke Marwa Mwita (42) ambao wote wamekatwa katika jiji la Dar es Saalm.


Sehemu ya Damu ya aliyekuwa Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza Barlow ndani ya gari aliyokuwa nayo siku ya kuuawa
Aidha DCI  Manumba alisema Kikosi kazi cha upelelezi kilichokuwa chini yake kilijigawa katika makundi matatu yaani la Ukamataji, Mahojiano na la interejensia huku wakitumia njia ya sanyansi kwa kufuatia mitandao ya simu.
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao wa dar na wale wa Mwanza kunafanya jumla yao kuwa 10 na bado jeshi linasaka wengine.  Lakini hakuna sababu iliyotokana na mauaji hayo ambayo imeelezwa mpaka sasa na jeshi hilo.
Wengine watano wanaoshikiliwa kwa                                                                                                                            usalama ni pamoja na Doroth Alicia Lymo (42) kabila mchaga ambaye ni Mwalimu wa shule ya Msingi Nyamagana  mkazi wa Kitangili Minazi mitatu Mwanza, ambaye alikuwa na marehemu siku ya tukio akisindikizwa,  Felix Felician Minde (50) kabila mhaya  mfanyabiashara mkazi wa Lumala na  Fumo Felician Minde (46) kabila mhaya mfanyabiashara mkazi wa kona ya Bwiru.Wengine katika orodha hiyo ni  Bahati Agustino Lazaro kabila Muha Mfanyabiashara mkazi wa Nyakabungo na Amos Weibe Magoto (Bonge) ambaye ndiye aliyekutwa na simu ya mwalimuDoroth
Chanzo:Gsengo Blog.