Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika mazungumzo na Gavana Jenerali wa Canada Mhe. David Johnson na mkewe Mama Sharon Johnson na viongozi wa serikali ya nchi hiyo katika jumba la Rideau jijini Ottawa, Canada, katika hatua yake ya kwanza ya ziara rasmi ya siku mbili jijini humo Jumatano Oktoba 4, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na watanzania waliojitokeza kumlaki, pembeni akiongozana na Gavana Jenerali wa Canada Mhe. David Johnson na mkewe Mama Sharon Johnson katika viwanja vya jumba la Rideau jijini Ottawa, Canada, katika hatua yake ya kwanza ya ziara rasmi ya siku mbili jijini humo Jumatano Oktoba 4, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Gavana Jenerali wa Canada Mhe. David Johnson katika mazungumzo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili rasmi katika viwanja vya jumba la Rideau Hall jijini Ottawa, Canada, katika hatua yake ya kwanza ya kuanza ziara rasmi ya siku mbili jijini humo Jumatano Oktoba 4, 2012. Jumba hilo ndilo makazi na ofisi rasmi ya Gavana Jenerali wa Canada tangia mwaka 1867 ambapo pamoja na kuishi humo pia hapo ndipo hutumika kwa kuwatunukia wananchi wa Canada waliofanya vyema, pa kupokelea wageni mashuhuri wa nchi za nje na pia ndipo anapofanyia shughuli zote za kitaifa akiwa kama mwakilishi wa Malkia wa Uingereza.