October 10, 2012

RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012 KATIKA KIJIJI CHA NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
 Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa kuzingatia Hadidu za Rejea Timu hiyo ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012. 

 Imewasilishwa na: John P. Mireny - Kiongozi wa Timu, MCT 
Hawra Shamte - Mhariri wa Siasa, Gazeti la Mwananchi, TEF
 Simon S. Berege - Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu Tumaini, Iringa

 ORODHA YA UFUPISHO 
CHADEMA – Chama cha DemokrasianaMaendeleo
 CPJ – Kamati ya Kutetea Waandishi wa Habari 
DCI - Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai

 IPC - Klabu ya Waandishi ya Iringa M4C - Harakati za Mabadiliko 

MISA - Taasisi ya Vyombo vya Habari ya Kusini mwa Afrika 
OC-CID - Mkuu wa Uchunguzi wa Makosa ya Uhalifu wa Wilaya

 OCD - Mkuu wa Polisi Polisi wa Wilaya RPC - Mkuu wa Polisi wa Mkoa TEF - Jukwaa la Wahariri Tanzania 

UNESCO - Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni .

Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012. 1.0 Muhtasari wa ripoti Ripoti hii ni ya wa uchunguzi mazingira yaliyopelekea kuuawa kwa Mwandishi wa Channel Ten Daudi Mwangosi mikononi mwa polisi katika kijiji cha Nyololo, wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa Septemba 2, 2012.

 Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kwa pamoja waliunda timu ya uhunguzi. Mchakato wenyewe ulihusisha mbinu za uchunguzi za kiuandishi wa habari ambazo si kama za uchunguzi wa kipolisi na wa kimahakama. Methodolojia za uchunguzi zilijumuisha mahojiano, kutembelea maeneo husika na uchambuzi mahsusi wa nyaraka kwa kuzingatia adidu za rejea zilizopo. Waandishi wa Habari waliokuwepo Nyololo na ambao hawakuwepo katika eneo la mauaji wametoa mchango muhimu. Mashahidi walioshuhudia katika kijiji cha Nyololo, wakiwemo watoto walikuwa vyanzo Muhimu. Habari zilizochapishwa katika vyombo vya habari kutokana taarifa rasmi kuhusu baa hilo pia zilichambuliwa kwa umakini. 

Uchambuzi mpana ulifanywa kuhusu hali ya mahusiano ya Uongozi wa Mkoa wa Iringa ( ikiwemo polisi) na wanahabari wa Iringa kabla ya mauaji ya Mwangosi.Mahusiano yalikuwa si mazuri na ya shaka kati ya pande hizo mbili tangu katika robo ya mwisho ya mwaka 2011. Hii ilisaidia kupata picha pana ya tatizo pamoja na kuweza kufahamu kwa undani tatizo lenyewe na kuweza kupanga mwelekeo wa uchunguzi wenyewe na hatimaye kuwezesha timu kuweza kuunganisha mambo na kuandaa ripoti hii. 

Aina nyingine ya ushahidi uliosaidia kuimarisha ripoti hii ni pamoja na video, picha mgando; maelezo kutoka katika mikutano na waandishi wa habari iliyofanyika Iringa na taarifa za vyombo vya habari. Mpaka wakati ripoti hii inaandikwa, taarifa rasmi kuhusu mauaji ya David Mwangosi zimekuwa zikitofautiana. Kwa kifupi matokeo ya mambo yaliyopelekea mauaji ya Daudi Mwangosi kwanza Yanadhihirisha bila wasiwasi kwamba Polisi kwa makusudi waliwaburuta waandishi waliotoka Iringa waliokuwa wakifuatlia habari za shughuli za Chadema katika kijiji cha Nyololo. Zaidi ya hapo, Daudi Mwangosi mwenyewe aliuliwa akiwa mikononi mwa polisi huku wakiangaliwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Michael Kamuhanda. 

 Uamuzi huu unadhihirishwa na ushahidi uliokusanywa kwenye maeneo pamoja na video na taarifa zingine za vyombo vya habari. 2.0 Tamko la Tatizo Kuanzia Machi 2012 mahusiano ya kikazi kati ya waandishi wa habari wa mkoa Iringa na viongozi wa utawala wa mkoa, ikiwemo jeshi la polisi, haukuwa mzuri. Katika mikutano yake mbalimbali ya kitaaluma, Klabu ya Waandishi Habari ya Iringa (IPC) kutoka katika robo ya mwisho mwaka 2011, waandishi wa habari wamekuwa wakilalamikia “kutotendewa sawa” na maofisa wanapokuwa wakifuatilia na kuandika habari mkoani Iringa. 

Kwa mfano , Novemba 2011, mwandishi Laurean Mkumbata anayeandikia ITV alipigwa vibaya na kamera yake ikaharibiwa na aliyekuwa mkuu wa polisi (OCD) wa wilaya ya Iringa , wakati mwandishi huyo alipokuwa kazini. Mkumbata alieleza mbele ya Timu ya Uchunguzi kwamba yeye na waandishi wengine akiwemo marehemu Daudi Mwangosi walikuwa wakikusanya habari katika mpambano kati ya polisi na kundi moja la watu mjini Iringa. Kundi hilo lilitaka kuchoma moto nyumba moja iliyodaiwa kuwa na wachawi ambao uwepo wao ulikuwa ukiathiri eneo lote jirani. Hali iliyojitokeza ni kwamba ofisa yule wa polisi alitaka kuharibu kifaa cha kazi cha mwandishi ili kuzuia upelekaji wa habari kuhusu mpambano wa wananchi wenye hasira na polisi. 

Wakati polisi walikuwa wakiwadhibiti watu hao kwa kutumia mabomu ya machozi na kufyatua risasi za moto hewani kuwatisha na kuwaondoa watu hao kutoka eneo la tukio, OCD Semunyu alimshika mwandishi huyo na kumnyang’anya kamera yake ambayo aliipiga chini mara tatu, na hivyo kuiharibu kabisa. Pamoja na hayo, Mkumbata alishikiliwa kwa muda alipokwenda kutoa taarifa kuhusu tukio hilo katika makao ya polisi ya mkoa. Baada ya hapo jitihada za kuficha ukweli zikaanza. Hata hivyo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa (RPC), Evarist Mangala aliingilia kati na kumwamuru ofisa aliyehusika, Semunyu, kulipa kamera iliyovunjwa. Ofisa huyo alitekeleza amri hiyo na Mkumbata alipata kamera yake.

 Ofisa huyo alilipa kutoka mfukoni mwake. Mkumbata anaamini kwamba ofisa yule wa polisi aliipiga chini kamera yake mara tatu kuhakikisha inaharibika kabisa na hakuna kinachopatikana, hatua iliyolenga kuhakikisha mwandishi huyo hawezi kutangaza taarifa za tukio kwa wakati. Tangu wakati huo hali ya kutiliana shaka imekua katika mahusiano ya wanahabari wa Iringa na Polisi. Mahusiano na viongozi wengine wa mkoa nayo hayajakuwa mazuri tangu kipindi hicho cha robo ya mwisho ya 2011.

 Frank Leonard, Katibu wa IPC anakumbuka kuwa mwishoni mwa Februari 2012, waandishi saba waliteuliwa na IPC kuandika habari ya ziara ya Makamu wa Rais mkoani Iringa, lakini walilazimika kulala ndani ya gari walilosafiria kwa kuwa maofisa wahusika wa mkoa walidaiwa kupuuza kuwapatia hoteli ya kulala. 

Tukio hilo liliudhi uongozi wa IPC ambao uliandaa maandamano ya amani kulalamikia unyanyasi wa waaandishi wa habari unofanywa na viongozi wa mkoa. Hatua hiyo, kwa mujibu wa Katibu huyo ililenga kuwasilisha kwa viongozi wa mkoa msimamo kwamba “Wanachama wa IPC hawaegemei chama chochote cha siasa, bali ni wanataaluma na wanaosimamia uandishi habari unaozingatia maslahi ya umma”. 

Machi 6, 2012, mamlaka ya polisi ya mkoa uliidhinisha ombi la IPC kuandamana kupinga kuendelea mahusiano yasiyo mazuri kati ya waandishi wa habari na uongozi wa mkoa. Katibu wa IPC anakiri kwamba mahusiano kati ya pande hizo mbili yaliboreka baada ya maandamano hayo ambapo aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa aliahidi kushughulikia tofauti zilizopo na kuhakikisha kunakuwa na maelewano.

  Kubadilika kwa mambo ghafla na kufikia mauaji ya Daudi Mwangosi hapo Septemba 2, 2012, wakati a akikusanya habari za shughuli za kisiasa za Chadema katika wilaya ya Mufindi , katika kijiji cha Nyololo mikononi mwa polisi wanaotuhumiwa kwa mauaji inastusha na ni jambo lisilo la kutegemewa kwa Frank Leaonard.

Marehemu Daudi Mwangosi alikuwa Mwenyekiti wa IPC. 3.0 Mamlaka Mamlaka ya uchunguzi huu inatokana na katiba ya Baraza la Habari Tanzania (MCT), kifungu 3 (e), kinachoelezea malengo ya Baraza kuwa ni: Kuwa na rejista ya matukio yanayoweza kukwaza upatikananji wa habari za manufaa kwa umma na muhimu, na kuchunguza tabia za watu, mashirika na vyombo vya serikali kwa ngazi zote dhidi ya vyombo vya habari, na kutangaza matokeo ya uchunguzi huo. 3.1 Lengo Lengo la uchunguzi huo ni kuweka rekodi sawa ya mazingira yaliyopelekea kuuawa kwa mwandishi wa Channel Ten na Mwenyekiti wa IPC, David Mwangosi , Septemba 2, 2012 katika kijiji cha Nyololo , wilaya ya Mufindi, mkoa wa Iringa .

 Uchunguzi huo ni huru na sio kama wa kipolisi au wa kimahakama lakini ni jitihada za dhati za kuweka kumbumbuku ya hali ya mambo kuhusu kifo cha kwanza cha mwandishi wa Tanzania akiwa kazini. 4.0 Adidu za Rejea Timu ya uchunguzi iliongozwa na Adidu za Rejea zifuatazo: 4.1 Lengo Kuu Kuchunguza hali iliyopelekea kuuawa kwa David Mwangosi. 4.2 Malengo mahsusi Kuchunguza chanzo cha kuwepo uhusiano usio mzuri kati ya IPC na uongozi wa kiutawala wa Iringa . Kuwahoji wanakijiji wa Nyololo kuhusu hali halisi iliyosababisha mapambano kati ya polisi/ Chadema/ waandishi wa habari. Kukusanya maelezo stahili kutoka kwa wananchi, IPC na mashuhuda waandishi waliokuwepo kwenye eneo la ghasia. 

Kuchambua kwa uhuru ripoti za vyombo vya habari, ripoti rasmi na za polisi na madai kuhusu tukio hilo. 5.0 Muda wa kukamilisha jukumu Kazi hiyo ilichukua siku nane (8) kuanzia Septemba 5, 2012 na kumalizika Septemba 12, 2012. 6.0 Methodolojia Timu ilianza uchunguzi kama ifuatavyo: Kwanza kabisa, hati na taarifa za magazeti kuhusiana na uchunguzi huo zilipitiwa ili kupata msingi wa suala hilo. Hii inajumuisha mamlaka ya kikatiba ya MCT kufanya uchunguzi kama huo. Pili, Timu hiyo imechunguza kwa karibu jinsi vyombo vya habari vilivyotangaza zikiwemo picha mgando, na video kuhusu kuuawa kwa Daudi Mwangosi hapo Septemba 2, 2012, na taarifa za awali za polisi dhidi ya mambo yaliyogunduliwa na wachunguzi katika uchunguzi wao. 

Taarifa zote zilizoripotiwa na polisi na Waziri mwenye dhamana kuhusu mauaji ya mwandishi kabla yataarifa ya kuundwa kwa kamati maalum ya uchunguzi ya Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi Septemba 4, 2012 yanachambuliwa kwa kina. Hatimaye, uchunguzi katika eneo. Hii ilihusisha kusafiri kwenda Iringa na kufanya mahojiano na watu walioteuliwa na wanahabari katika kijiji cha Nyololo waliokuwepo siku Mwangosi. 

Utaratibu wa mahojiano ya mtiririko kutokana na majibu ulitumiwa na wachunguzi kwa watu mbalimbali. Utaratibu mkuu ulikuwa ni mazungumzo ya bayana kati ya wachunguzi na watu mbalimbali wakiwemo baadhi ya wanakijiji wa Nyololo. Mbinu za kiuchunguzi za uandishi wa habari zilitumika kufanikisha lengo la jukumu hilo.Matokeo yake, mchakato huo uliwezesha kupatikana ukweli uliowezesha kukamilisha ripoti. 7.0 Matokeo 7.1 Maelezo ya awali Hapo Septemba 2, 2012, mikutano miwili tofauti ya waandishi wa habari iliyosheheni ilifanyika katika Manispaa ya Iringa kwa nyakati tofauti siku hiyo. 

Mkutano wa kwanza uliitishwa na kuhutubiwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa (RPC), Michael Kamuhanda katika ofisi yake asubuhi. Mada ya mkutano huo ni uamuzi wa polisi kuzuia mikutano ya kisiasa iliyopangwa na chama cha upinzani cha Chadema katika mkoa wa Iringa iliyolenga kutelekeza kampeni za chama hicho za Kuleta Mabadiliko nchi nzima. 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa alitahadharisha kuwa sensa ya watu na makazi ambayo awali ilikuwa ilipangwa kufanyika Agosti 26 – Septemba 1, 2012, imeongezewa muda na serikali hadi Septemba 8, 2012, na mikusanyiko ya kijamii na mikutano ya kisiasa imesimamisha mpaka zoezi hilo likamilike. Waandishi wa habari waliokuwepo kwenye mkutano huo wanakiri kwamba katika mkutano huo marehemu Daudi Mwangosi alikuwa ni ripota pekee aliyemuuliza RPC “maswali magumu” kiasi cha kumkera kiongozi huyo wa polisi. 

Mojawapo ya maswali yaliyoulizwa na Mwangosi ni ufafanuzi sahihi wa nini hasa ni “ mkutano wa ndani wa chama” kulingana na madai ya maofisa wa Chadema kwamba chama hicho hakipangi kufanya mikutano ya hadhara na maandamano ya kisiasa bali ni kufungua matawi mkoani Iringa bila kufanya mikutano. Katibu wa IPC anakumbuka swali moja la Mwangosi kwenye mkutano huo ambalo lilimuudhi RPC. Aliuliza: kwanini chama tawala cha CCM kiko huru kufanya mikutano ya kisiasa wakati chama cha upinzani kama Chadema kinawekewa vikwazo na polisi kila wakati. Wakati marehemu Mwangosi akisisitiza ufafanuzi zaidi kutoka kwa Mkuu huyo wa polisi wa mkoa, RPC alisisitiza : “ Hii ni amri na polisi hairuhusu maswali zaidi kuhusu suala hili”. 


Na taarifa kutoka kwa RPC imewakumbusha wazi wanasisasa, vyama vya siasa na wananchi kwa jumla kwamba “mikutano ya vyama vya kisiasa imezuiliwa kutokana na kuendelea kwa sensa ya watu na makazi kwa siku saba zaidi kuanzia Septemba 2, 2012. Mara baada ya mkutano na RPC baadhi ya maofisa wa polisi walionyesha kuwa mambo hayatakuwa sawa katika kijiji cha Nyololo village Waandishi wengine wa Iringa, Clement Sanga anayeandikia magazeti ya Mwananchi Communications Ltd na Oliver Motto, mwandishi wa kujitegemea wa gazeti la Mtanzania, Star TV na Radio Free Africa walisema haya : “Baada ya mkutano huo na waandishi , wakati wanahabari wakitoka kwenye ofisi za mkoa za Polisi, baadhi ya polisi walisikika bila wao kuwa wakiwaonya wasiende Nyololo kwa ajili ya kukusanya habari za shughuli za siasa za Chadema kutokana na kuwa na uwezekano wa hatari”. 

Mkutano wa pili wa waandishi uliitishwa mchana na Chadema na ukahutubiwa na Katibu Mkuu na Dk.Wilbroad Slaa na kamanda wa Kampeni ya Mabadiliko ya chama hicho Benson Kigaila. Katika mkutano huo , Chadema ilichachamaa na kutetea kampeni zake za mabadiliko na kushutumu polisi kwa kufanya njama za kuzima kamepni hizo.

 Chadema ilihoji kwanini polisi inabagua vyama vya upinzani wakati wakipendelea chama tawala CCM kwa madai ya kusimamia sheria. Licha ya kuwepo amri ya polisi ya kuzuia mikutano yote ya siasa mpaka zoezi la sensa ya watu na makazi lililoongezewa muda limalizike , Chadema ilidai kwenye mkutano huo kwamba kampeni za uchaguzi za CCM katika uchaguzi mdogo ziliruhusiwa kufanyika katika jimbo la Bububu , Zanzibar. Kampeni za uchaguzi mdogo wa Bububu zilizinduliwa Jumapili Septemba 2, 2012 na Makamu wa Rais wa serikali ya Muungano, Dk. Mohammed Gharib Bilal. Hivyo kwa ufupi, Chadema iliamua kuendelea na kampeni zake mkoani Iringa , ikiwemo kufungua matawi ya chama katika kijiji cha Nyololo, wilaya ya Mufindi Jumapili Septemba 2, 2012, lakini bila kufanya mikutano ya hadhara. Hatimaye maofisa walishikilia msimamo wao na kuendelea kufufungua matawi ya chama Nyololo.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa Iringa, RPC Michael Kamuhanda, alipanga askari wake kwenye magari ya wazi kufuatilia msafara wa maofisa wa Chadema. Pande hizo mbili zilikutana kwenye kijiji cha Nyololo. Viongozi wa Chadema walipanga kufungua matawi mawili katika kijiji cha Nyololo village, kiasi cha kilomita 500 (315 maili) magharibi mwa Dar es Salaam, na mwendo wa saa tatu kwa gari kutoka Manispaa ya Iringa. 

Matawi hayo yako umbali wa kilomita tatu kutoka kila moja yakitenganishwa na barabara kuu ya Dar es Salaam -Tunduma. Mchoro uliopo ukurasa wa 16 unaonyesha hali halisi ilivyokuwa, kama ilivyoelezwa na mashuhuda waliokuwepo na kuboreshwa na wachuguzi.

 Kwa lengo la kuonyesha , maeneo mawili yamewekewa alama tofauti ya A ikimaanisha “eneo tulivu” na B ikimaanisha “eneo la umwagaji damu”. Katika eneo la [A], ambapo utulivu ulikuwepo na ulizingatiwa na polisi katika maamuzi na matendo yao ambapo vurugu na umwagaji damu uliepukwa. 

Eneo lingine ni [B], ambapo polisi ilitumia, nguvu zaidi na kupelekea mauaji ya Daudi Mwangosi na kujeruhi waandishi wengine kadhaa wa Iringa na makada wa Chadema. 7.2 Eneo la matukio ya utulivu [A] Hapa ni sehemu ya kwanza lilipo tawi la Chadema kusini mashariki mwa barabara ya changarawe inayopita kijiji cha Nyololo, kutoka barabara kuu ya Dar-Tunduma. Mashuhuda (waandishi na wanakijiji) wal;isema kuwa baada ua kuwasili kwenye eneo la tawi, maofisa wa Chadema na wanachama walishuka kutoka kwenye magari wakiwa tayari kuanza shughuli. Ukanda wa njano uliwekwa kuzunguka ofisi ya Chadema kuzuia watu kukusanyika katika jingo la ofisi hiyo. Mara baada ya Chadema kuanza mkutano wao wa ndani kikundi cha askari wa kikosi cha kuzuia fufo (FFU) kilifika eneo hilo na kujipanga kwa muundo wa kijeshi wa V. Kikosi hicho kilikua chini ya uongozi wa Ofisa wa kudhibiti uhalifu wa mkoa (RCO) SSP Nyigesa Wankyo.

 Kamanda wa kikundi cha FFU OC Florent Mnunka anaamuru polisi wainue bendera nyekundu yenye maandishi ya kuwataka watu waliokusanyika kutawanyika ama vinginevyo watatumia nguvu. Kamanda huyo anatangaza “Watu wote mliokusanyika hapa, mnaamriwa na Jamhuri ya Muungano ya Tanzania mtawanyike mara moja na kwa amani, vinginevyo tutatumia nguvu ” anarudia maneno hayo 

 Baada ya kurudia amri hiyo mara tatu, OC-CID anaamuru polisi kusogea karibu na ofisi ya Chadema. Wakati wakisogelea eneo hilo la Utulivu [A] , Kamanda wa kampeni ya mabadiliko ya Chadema Benson Kigaila na viongozi wengine walitoka nje ya ofisi hiyo na kumuomba kamanda wa FFU kuzuia askari wake kutumia nguvu bila sababu kwa kuwa haikupanga kufanya mkutano wa hadhara wa kisiasa. Viongozi wengine waliokuwa na Kigaila walikuwa ni Alfred Lwakatare na Naibu Katubu Mkuu wa Chadema Zanzibar , Said Issa Mohamed. 

Pande hizo mbili zilipingana kwa muda kuhusu maana sahihi ya“ mkutano wa ndani wa chama” na kama maana yake ni tofauti na mikutano iliyozuiwa na polisi . Ushahidi wa picha za video uliopatikana na waandishi wa habari wengi unadhihirisha na kuonyesha mvutano kati ya polisi na Chadema katika eneo tulivu[A] kama ifuatavyo: Benson Kigaila: “ Sisi tuko katika ofisi ya tawi letu, tunajua sheria , hili ni tawi la Chadema”. Kamanda wa FFU : “Tunawaonyeni nyingi, tafadhali, fanyeni mkutano wenu ndani ya ofisi” Benson Kigaila: “Hatuendi kokote ” Kamanda wa FFU: “Ingieni ndani” Ghafla RCO akaingilia na kushauri viongozi wa Chadema kuwaambia wananchama wao waingie ndani ya ofisi yao..

Wanachama walikubali lakini wote wasingeweza kutosha kwa sababu ofisi yenyewe ni ndogo. . RCO akasisitiza: “Huu ni mkutano usioruhusiwa, tafadhali ingieni ndani” Mwenyekiti wa Taifa wa vijana wa Chadema (Bavita), John Heche akajibu : “Tatizo ni nini? Kama mmetumwa kuua, fyatueni risasi na muue…sisi tutakaa hapa.” Kijana mmoja wa Chadema anasikika katika video akiwaambia polisi ; “Jana makada wa CCM walirejesha fomu za uchaguzi wa chama chao kwa maandamano na sherehe … sisi hatuko tayari kuondoka ”. 

John Heche anabishana na polisi akisema : “Mfahamu sheria zenu kabla ya kufanya kazi yenu” Mwishowe, maelewano yalifikiwa kati ya RCO na maofisa wa Chadema ,na kamanda anaamuru maofisa wake kutotumia nguvu dhidi ya watu waliokusanyika kwenye ofisi ile. Ofisa mmoja wa Polisi analalamika , “Wanatupotezea muda wetu ….aaah wanachukua muda wetu”. Ofisa huyo inaelekea alikuwa akilalamikia amri ya mwisho iliyotolewa na mkuu wake, RCO, ikikitaka kikisi hicho kuacha kutumia nguvu, ikiwa inakiuka amri awa awali. 

Waandishi dhidi ya RPC Kamuhanda Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Michael Kamuhanda anawasili kwenye eneo la utulivu [A] dakika chake baada ya RCO, maofisa wa FFU na wa Chadema kufikia muafaka na kukubaliana kuhusu maana ya “mkutano wa ndani”. Waandishi waliokuwepo eneo hilo walimpokea kwa maswali kadhaa kuhusu tofauti za polisi na Chadema. Marehemu Daudi Mwangosi akiwa mmoja wa waandishi hao waliomkabili RPC. Mwangosi alimuuliza RPC: “Watu hawa wako katika eneo la ofisi yao, kuna tatizo lolote linalotokana na shughuli wanazokusudia kufanya?” RPC anamjibu Mwangosi “Nimeshakuambia usiwe mbishi. 

Nilichokuambia ni kwamba nimezuia mikutano yote ya kisiasa…Lakini usije na mambo yale yale asubuhi, jioni na mchana, na jua linapozama…kuna umuhimu gani kutuuliza sisi tupo hapa kufanya nini?”. Mwandishi mwingine (Jina lake halikutapitkana ) “Nafikiri wewe ndiye mbishi (RPC)” RPC “Nilichozuia ni mikutano ya hadhara ya kisiasa, lakini shughuli zote za ndani zinaruhusiwa kuendelea…hadi sasa hakuna tatizo” RPC anaendelea: “Tumefanikiwa kuzuia mikutano na ghasia… kama wanataka kufanya mikutano ya ndani wanaweza kuendelea.” Mwangosi “…kama wanavyofanya sasa …..…” RPC anajibu, “Kama walivyofanya tangu juzi ” Baada ya kubadilishana maneno zaidi RPC anasema:

 “Tunawataka viongozi, hatutashughulika na watu waliokusanyika hapa. Lengo letu ni kushughulikia walioitisha mkutano… wao ndio chanzo cha kila kitu, na wanavunja amri rasmi”. Tunaogopa kuwajeruhi watu bila sababu, hivyo tutashughulika na viongozi ambao ni kundi dogo na ni rahisi kulishughulikia” anasema RPC na kuamuru “Sasa hakuna mkutano, huu (mkusanyiko) unaofanyika nje.” Mwangosi anaingilia: “ 

Huu ni mkutano ? RPC anaamuru mkusanyiko kuendelea na mkutano wao ndani; “Ingia ndani” Mwandishi ( anayetambulika kwa kubeba kamera na akiwa katika kundi la waandishi): “Inakuwaje kama chumba ni kidogo kutosha watu wote?” RPC: “Tutawakamata ninyi viongozi kama mtaendelea ”Sauti ya mtu anayedhaniwa kuwa kiongozi wa Chadema inasema: 

“Tutaendelea kuwapo hapa .” RPC: “Ndiyo na ninyi mko wachache, tunawamudu ” Mtu huyo anajibu : “Aah! Hamna tatizo… ni miaka mingapi Mandela alikaa gerezani ”? RPC anajibu , “ Hata miaka 30, lakini umemtaja Mandela, wewe Mandela?” Wakati waandishi wakimhoji RPC, maofisa wa Chadema waliendelea na mkutano wao na kuumaliza kwa amani. Chadema walimaliza shughuli yao na wanahabari wakafanya kazi yao hapa bila kunyanyaswa. Baaada ya hapo makada wa Chadema walipanda basi lao kwenda kaskazini magharibi kwenye ofisi nyingine. 

Katika eneo hili la utulivu. [A],mabomu ya machozi hayakulipuliwa wala risasi hazikupigwa kuwatisha watu. Pia hakuna mtu aliyeuawa. 7.3 Eneo la umwagaji damu [B] Mara baada ya maofisa wa Chadema kumaliza ufunguzi wa tawi katika eneo la utulivu [A], walikwenda kukamilisha shughuli katika eneo la umwagaji damu [B]. Inachukua chini ya dakika 20 kutembea kufika katika ofisi ya pili ya Chadema. wakati maofisa wa chama wakielekea katika eneo hilo, polisi waliwafuata kwa karibu. Waandishi wa habari pia waliwafuatilia ili kukusanya habari za shughuli hiyo. Lakini kitu kimoja kibaya kilitokea hata kabla ya askari wote wa FFU kufika katika eneo la Umwagaji damu [B]. 

Mashuhuda wanaeleza kuwa RPC alimwita RCO na kumuonya wazi kuhusu “ kushughulikia kwa amani’ masuala ya Chadema katika eneo la awali la utulivu [A]. Inaelekea RCO alijitoa kuelekea eneo la umwagaji damu [B], na hivyo usimamizi wa utoaji maamuzi katika Eneo la Umwagaji damu [B] ulibakia kwa mkuu wake ambaye ni RPC Michael Kamuhanda. Mabishano na waandishi wa habari kama yaliyotokea katika eneo la la awali yaliibuka tena. Hapa makada wa Chadema walikusanyika nje ya ofisi yao wakiimba t“Wamezoea kuua , wamezoea kuua”.

 Inaelekea wimbo huo uliwaudhi polisi. Vurugu zikaanza pale RPC alipoamuru kukamatwa kwa viongozi wa Chadema waliokuwepo, kwa mujibu wa watu walioshughudia. Kufuataia amri hiyo ya RPC kulingana na mashuhuda , polisi kwanza waliingia kwa nguvu katika ofisi ya Chadema, wakipiga mabomu ya machozi na kuaamuru viongozi hao wajisalimishe. 

Baada ya polisi kutumia nguvu, kiongozi wa kampenu za mabadiliko wa Chadema mkoani Iringa, Benson Kigaila , aliwaomba wafuasi wachache wa chama hicho na viongozi waliokuwepo kujisalimisha kwa kuketi na kuinua mikono yao juu”. Waandishi wawili waliohojiwa, Clement Sanga wa Mwananchi Communications Ltd na Oliver Motto, mwandishi wa kujitegemea wa Mtanzania, Star TV na Radio Free Africa walishuhudia ghasia hizo katika kijiji cha Nyololo village, wakati wakiwa wamekimbilia sehemu ya barabarani, hatua chache kutoka eneo hilo la umwagaji damu .


  Waandishi hao walisema kuwa wakati makada wa Chadema walitii maagizo ya viongozi wao ya kuketi na kuinua mikono yao juu, polisi walifyatua risasi na n a mabomu ya machozi, na kuwapiga makada hao na waandishi kwa virungu. 7.4 Matukio yasiyo ya kawaida katika Eneo la Umwagaji Damu (B) Jambo moja la kushangaza katika eneo la umwagaji damu B ni kuwepo kwa raia wachache (makada wa Chadema na waandishi kwa pamoja), wakiwa wamezidiwa kabisa na idadi ya polisi. Maelezo ya mashuhuda, picha mgando na video zinadhihirisha hii bila shaka yoyote. 

Wanakijiji wa Nyololo waliohojiwa walisema kwamba Jumamosi Septemba 1, 2012 watu wanaoaminika kuwa ni askari kanzu walifika eneo hilo na kuwaonya wakazi wake kuhusu ya hatari inayowza kutokea kama wakihudhuria shughuli za ufgunguzi wa matawi ya Chadema. Walidai kuwa walishauriwa pia kuondoka katika maeneo yao wakati wa saa za mchana Jumapili Septemba 2, 2012 wakati ambao Chadema imepanga kuendesha shughuli zake. Mkakati wa kutisha ulifanikiwa kwa sababu watu wazima wakazi wa Nyololo waliohojiwa baadaye walisema hawajui kuhusu vurugu za polisi na Chadema kwa sababu walitelekeza ushauri wa kuondoka katika maeneo hayo. Mwanamke mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema:: 


“Nimejua kuhusu ghasia hizo na kifo cha mwandishi wa habari kijijini kwetu baada ya kurejea nyumbani jioni.” Kutokana na uvumi wa vitisho uliosambazwa Jumamosi Septemba 1st, 2012, nilipanga kumtembelea jamaa yangu aliye mbali kama njia ya kuepuka”. 7.5 Mauaji ya David Mwangosi Baada ya kumaliza ukusanyaji wa habari kwa amani katika enelo la utulivu [A], waandishi wa habari walikwenda katika eneo ambalo liligeuka kuwa mtego wa kifo Eneo la Umwagaji damu [B] kutoka mwelekeo wa kusini mashariki kupita barabara kuu ya Dar-Tunduma kumalizia kazia yao. Alipoangalia nyuma , Daudi Mwangosi aliona kikundi cha polisi wakimpiga mwandishi mkuu wa gazeti la Nipashe, wa Iringa, Godfrey Mushi (32).

 Mwandisi huyo alipigwa mpaka akapoteza fahamu na akapata fahamu akiwa kwenye kituo cha polisi cha Mafinga. Kamera yake, daftari lake na kalamu havikupatiakana. Wakati mwandishi Godfrey Mushi akiwa bado anapigwa na polisi, marehemu Mwangosi aliwakimbilia akiwaomba waache kumdhuru zaidi Mushi kwa kuwa alikuwa mwandishi tu. 

Polisi hawakumsikiliza. Badala yake wakamburuta mwandishi huyo ambaye tayari alikuwa amepoteza fahamu na kumweka kwenye gari lao na wakamgeukiwa Daudi Mwangosi mwenyewe, kwa vurugu na mabmu ya machozi, na kwanza akapoteza fahamu. Baada ya kuona hivyo, Addallah Said mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima akamkimbilia RPC ambaye alikuwa katika gari lake la polisi aina ya Land Cruiser kumuomba awaamuru askari waache kumpiga mwandishi Daudi Mwangosi. Wakati huo huo, inaelekea kutokana na kushangazwa na polisi kumpiga kinyama Daudi Mwangosi, Mkuu wa polisi wa Mafinga OCD Asseri Mwampamba, aliamua kuingilia , kwanza kwa kuwaamuru na kuwaomba askari waache kumpiga marehemu Mwangosi.

 Mwandisi wa ITV, Renatus Mutabuzi ambaye alirekodi tukio hilo “laivu” alithibitisha kwa timu ya wachunguzi kuwa licha ya jitihada za OCD Asseri kuingilia na kumlinda Mwangosi kutokana na kipigo, polisi hao hawakumsikiliza. Wakati polisi wakiendelea kumpiga Mwangosi, alijaribu kujiokoa kwa kumkumbatia OCD Asseri Mwampamba, na baadaye kumwangukia miguuni mwake kuepuka kipigo zaidi. Baadhi ya waandishi wa Iringa waliokuwa wamejificha waliweza kupiga picha za mgando na pia za video za vurugu hizo. Waandishi kutoka Dar es Salaam waliweza kukusanya habari za vurugu hizo kwa sababu tofauti na wenzao wa Iringa, polisi hawakuwalenga. Mwanamke ambaye alijeruhiwa katika vurugu hizo, aliyekuwepo kwenye eneo hilo la umwangaji damu B alisema kuwa alilala karibu na ambapo Daudi Mwangosi aliuawa ili kuepuka kipigo zaidi kutoka kwa FFU.

 Alizungumza na timu ya uchunguzi kwa sharti la kutotajawa. Mwanamke huyo anadai kuwa aliangalia na hata alimsikia mwandishi Addallah Said akikikimbilia gari la RPC na kumuomba awaamuru askari wasiendelea kumpiga Daudi Mwangosi. Alijeruhiwa vibaya na alilazwa kwenye hospitali ya wilaya ya Mafinga kwa siku tatu. RPC hakutekeleza ombi la mwandishi huyo.

 Badala yake alifunga kioo cha gari lake . Sekunde chache baadaye gari lake lilipiga honi na wakati huo huo mlipuko wa bomu la machozi ukasikika na kumua mara moja Daudi Mwangosi. Kwa sababu marehemu Mwangosi alikuwa bado chini ya miguu ya OCD Asseri Mwampamba, naye pia alijeruhiwa katika mlipuko huo. Picha za mgando zinaonyesha polisi akipiga bomu la machozi tumboni mwa Daudi kwa karibu kabisa. 

Kwa masikito makubwa, mwanamke huyo anasema alijua kabisa Daudi Mwangosi ameuawa mbele ya RPC Michael Kamuhanda. Kwa Addallah Said na yule mwanamke , kupigwa kwa honi na kutokea kwa mlipuko kwa wakati mmoja bado ni kitendawili. Kwa kutoamini kilichotokea, , OCD Asseri Mwampamba alilalama kwa uchungu kutokana na mlipuko wa bomu la machozi akisema: “Sasa,umefanya nini ”? 7.6 Taarifa rasmi zinazokinzana Taarifa rasmi lakini zinazokinzana za polisi kuhusu kuuawa kwa David Mwangosi zilipatikana kwa vyombo mbalimbali vya habari kuanzia Septemba 3, 2012.

 Mamlaka rasmi hazijafuta taarifa hizo mpaka wakati wa kuchapisha taarifa hii. Taarifa hizo, vyanzo maalum na vyombo mbalimbali vya habari vilivyoandika habari hizo vinaorodheshwa kama ifuatavyo: Taarifa rasmi kwa vyombo vya habari Taarifa (s) Mwangosi afariki kutokana na kitu kizito kilichotupwa na waandamanaji 

• Polisi wakanusha kuhusika moja kwa moja na kifo cha mwandishi • Uchunguzi wa pamoja wa Polisi na Jeshi utafanywa kutokana na kifo cha mwandishi. 

• Baada ya kuvunjwa kwa ghasia, Mwangosi anakimbilia walipo polisi na kitu kama bomu kikarushwa kundi la watu wanaokimbia na kumlipua Mwangosi. 

• Watu kadhaa wengine walijeruhiwa wakiwemo polisi. 

• Siko katika nafasi ya kuzungumza kwa sababu sasa hivi niko katika chumba cha maiti cha hospitali ya mkoa ya Iringa. 

• Akanusha kuthibitisha kifo lakini athibitisha mtu mmoja amekufa.

 • Athibitisha kifo cha mtu mmoja lakini hana uhakika kama aliyekufa ni mwandishi wa Channel Ten Chanzo RPC wa Iringa Michael Kamuhanda Kamishna wa Operesheni wa Polisi Paul Chagonja Taarifa zimepatikana kutoka Polisi makao makuu RPC wa Iringa Michael Kamuhanda RPC Michael Kamuhanda Chombo cha habari / Tarehe/Toleo Na. 

• Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari (CPJ). 3/09/2012 Mtandao 

• Matangazo ya Channel Ten, asubuhi ya Septemba 3, 2012 Reuters 4/09/2012 mtandao Habari Leo 03/09/2012 02083 1-habari kiongozi Uk. 1

 • Matangazo ya Channel Ten asubuhi ya Septemba 3, 2012 The Daily News 3/09/2012 10726 Habari kuu Gazeti la Nipashe linanukuu Channel Ten

 • RPC anakataa kuzungumza akisema alikuwa kwenye mkutano • Akanusha madai kuwa polisi wamemuua mwandishi. • 

Kilichosababishakifo ni kitu kilichorushwa na kundi la watu. Polisi wanachunguza.

 • Polisi ilikuwa ikitawanya kundi la watu. Mwandishi alikuwa akikimbia kutoka kundi la watu akifuata polisi. Kitu hicho pia kilijeruhi watu wengine na baadhi ya maofisa wa polisi akiwemo OCS.

 • Hawatachukua muda mrefu kukamiklisha uchunguzi kwa sababu mashahidi wengi wanajulikana.

 • Mwili wa Mwangosi umechukuliwa kwa uchunguzi • Mwandishi aliuawa na bomu la machozi ambalo halikuwa limeshughulikiwa vizuri na polisi • 

Hatutakuwa katika nafasi ya kusema nani anahusika na mauaji hayo timu mbili za uchunguzi zitakapokamilisha kazi zake. Hapo ndipo hatua za kisheria zinapoweza kuchukuliwa. 

Msemaji wa polisi Advera Senso Mkurugenzi Mkuu wa Upelelezi DCI Robert Manumba Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi (alikariri na Katibu Mtendaji wa Baraza la Habar Tanzanika (MCT) Kajubi Mukajanga) Dk. Emmanuel Nchimbi – Waziri wa Mambo ya Ndani Gazeti la Nipashe 03/09/2012 03/09/2012 Habari kuu Gazeti la Mwananchi 03/09/2012 Habari Kuu The Daily News 04/09/2012 Uk. Wa kwanza habari ndogo Habari Leo 04/09/2012 02084 Habari Kuu Daily News 05/09/2012 10, 728 Habari ya pili kwa ukubwa (mbele) 7.7 Taarifa rasmi katika muktadha Kwa upande mmoja Waziri wa Mambo ya Ndani anakiri 4/09/2012 kwamba Daudi Mwangosi aliuawa na bomu la machozi ambalo halikuwa limeshughulikiwa vizuri, siku inayofuata RPC wa Iringa anatokea kwenye televisheni akitangaza habari za kuwatupia lawama wafuasi wa Chadema kwa kutupa kitu kizito kilicholipuka na kumuua Mwanjisi, kujeruhi watu kadhaa wakiwemo maofisa wa Polisi. 

Mashuhuda na mambo kadhaa yaliyochukuliwa kwa video na picha mgando zinaonyesha kuwa hakukuwa na kundi la watu bali ni wanahabari na baadhi ya viongozi wa Chadema ambao walikuwa wachache kulinganisha na idadi ya polisi. 

Hata hivyo RPC anadai kuwa kuiikuwa na kundi la watu wakifanya vurugu. Pia polisi na taarifa zingine rasmi zimeacha kueleza kuwa tukio la ufunguzi wa tawi lilifanyika katika eneo tulivu A bila ghasia. Septemba 12, 2012 Konstebo wa Polisi, Cleophase Pasifious Simon (23) alifikishwa mahakamani kwa akituhumiwa kwa mauaji ya Mwangosi. .Ushahidi unaonyesha kuwa marehemu Mwangosi alikuwa amezingirwa na akipigwa na polisi wasiopungua saba.


 Polisi mmoja akiwa amelenga bunduki la kupigia bomu la machozi tumboni mwa Mwangosi. Kukamatwa kwa Konstebo wa polisi na kushitakiwa kunathibitisha Waziri wa Mambo ya Ndani alichomwambia Katibu Mtendaji wa MCT kuhusu bomu la machozi “kutokushughulikiwa vizuri” kinyume na jitihada za kuficha ukweli za RPC wa Iringa, Michael Kamuhanda na maofisa wa polisi wa makao makuu ya polisi mjini Dar es Salaam. Cha kushangaza, wakati akihutubia mkutano wa wanahabari uliovunjika mjini Iringa Septemba 5, 2012 , Mkurugenzi wa Upepelezi wa Makosa ya Jinai, (DCI), Robert Manumba alisema “matukio ya aina hii yapo na yataendelea kutokea”. 

Matamshi haya yalitangazwa sana na vyombo vya habari. Manumba alikuwa akijaribu kuwasihi wanahabari wa Iringa ambao waligomea mkutano aliouitisha mpaka maofisa wote wa polisi wa Iringa waondoke kwenye ukumbi waliokuwemo. 

Mgomo huu ulichukuliwa kufuatia uamuzi wa IPC kugomea kuandika habari za polisi mkoani humo mpaka uchunguzi kuhusu kuuawa ukamilike Daudi Mwangosi. 8.0 Iliyobaki yote ni historia Kilichowashangaza waandishi katika hatua hii ni kwamba ghafla polisi waliwageuka. Hata baada ya kuona kuwa mambo yamekuwa mabaya na kukimbia kujifisha kwenye vichaka vya karibu, polisi waliwafuata na kuwalenga kwa mabomu ya machozi huku wakikimbia.

 Francis Godwin, mwandishi wa kujitegema, shuhuda na Naibu Katibu Mkuu wa IPC anakumbuka kuwa polisi wawili walimfukuza mpaka kwenye vichaka vya kijiji cha Nyololo ambapo alilazimika kuacha gari lake na kurejea usiku kulifuata. Wakiwa katika sehemu walipojificha, waandishi walikuwa wakimsaidia Abdallah Said kuondoa vipande vya nyama ya binadamu vilivyompata kutoka katika mwili wa Daudi Mwangosi. 

Baada ya mkutano wa waandishi wa habari wa asubuhi katika ofisi za RPC, waandishi waliokuwepo wanakumbuka kuwa askari mmoja mpelelezi alimfuata Mwangosi na kumwambia : “Ina maana gani kwenda Nyololo kuandika habari za shughuli za Chadema ambazo zinaweza kuishia na kifo chako”? Akiwa anatabasamu, Mwangosi alisema: “ nikifa leo , mwili wangu hautazikwa ardhini lakini katika mioyo ya watu”. 

Ilikuwa kama vile anatabiri kifo chake. Katibu wa IPC Frank Leonard haelewi kwanini polisi waliwageuka wandishi wenzake. “Kila siku saa tano asubuhi , tunashiriki katika mkutano wa waandishi wa habari unaoitishwa na RPC ofisini kwake. Sisi na maofisa wake tunajua sana na hata kwa majina. Ni kitendawili kikubwa Polisi wamewashambulia waandishi wakiwa kazini na hatimaye kumuua Daudi Mwangosi”. 

Katika eneo moja [A], kulikuwa na utulivu ambapo vurugu na umwagaji damu haukuwepo ambapo katika eneo lingine [B], polisi walitumia nguvu ya ziada, kupelekea kuuawa kwa Daudi Mwangosi na kujeruhiwa makada wengine kadhaa wa Chadema. 9.0 Shutuma na kulaaniwa kwa hapa nchini na kimataifa MCT Baraza la Habari Tanzania (MCT) limelaani vikali tukio hilo ambalo ni tishio la moja kwa moja kwa uhuru wa vyombo vya habari. 

“Hili ni tukio la kwanza kwa mwandishi wa habari kuuawa akiwa kazini”, Katibu Mtendaji wa alikaririwa na vyombo vingi vya habari akisema. MCT inataka mamlaka husika kufanya kila liwezekanlo kuhakikisha kuwa ukweli wa kilichotokea katika siku ya mauaji hayo ya kikatili unajulikana. 

MCT imeshutumu kuwahusisha wanahabari na shughuli za kisiasa na kumuhusisha na chama cha siasa wakati alikuwa akifanya kazi yake UTPC Taarifa ya Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC)umeshutumu vikali mauaji ya Daudi Mwangosi mikononi mwa polisi wakati akitekeleza kazi zake kama mwandishi wa habari. Taarifa hiyo imeitaka serikali kuwawajibisha mara moja polisi waliohusika na operesheni iliyopelekea kifo cha Mwangosi.

 UTPC imetaka kufukuzwa kazi mara moja kwa maofisa waliohusika na kifo marehemu Daudi Mwangosi. Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limelaani vikali mauaji ya Mwangosi mikononi mwa polisi. Katibu Mkuu wa TEF, Neville Meena, anasema hii ni mara ya kwanza katika historia ya sasa Tanzania kwa mwandishi kuuawa akiwa kazini. MISA na wengine Taasisi ya Vyombo vya Habari ya Kusini mwa Afrika (MISA), Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari (CPJ) na ARTICLE 19, zote zimelaani kuuawa kwa Daudi Mwangosi akiwa mikononi mwa polisi. 

Levi Kabwato, ofisa Programu wa MISA anayeshughulikia Ufuatiliaji wa Uhuru wa Vyombo vya Habari na Utafiti, alieleza katika taarifa kustushwa kwake na mauaji ya Mwangosi. “Hii inastusha. Septemba 2 2012, si siku mbaya kwa uandishi wa habari wa Tanzania bali kwa eneo zima na dunia yote. Ghasia siyo jibu, hazitatui kitu.

 Tunaitaka serikali ya Tanzania kuanzisha uchunguzi na kuwawajibisha wote waliohusika na upotefu wa maisha,” Kabwato alisema katika taarifa. CPJ inasema kwamba kifo cha Mwangosi ni cha kwanza kwa mwanahabari aliye kazini nchini Tanzania tangu taasisi hiyo ilipoanza kuweka rekodi za kina 1992 ARTICLE 19 imeeleza kusikitishwa na mauaji ya Daudi Mwangosi mikononi mwa Polisi wa Tanzania, na kuitaka serikali ihakikishe wote waliohusika wanashitakiwa. Unesco Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Irina Bokova, pia alishutumu mauaji ya mwandishi wa habari wa Tanzania, Daudi Mwangosi Septemba2, 2012 na kuitaka serikali kuchunguza mauaji hayo. UNESCO inataka serikali ichunguze kifo hicho na kuwashitaki wote wanaohusika. 

Taarifa ya UNESCO inasema: “ Ni muhimu kwa demokrasi na utawala wa sheria kwamba waandishi waruhusiwe kufanyakazi zao na kutumia haki yao ya kujieleza kwa usalama.” 10.0 Hitimisho na Mapendekezo Mauaji ya David Mwangosi mikononi mwa polisi wakati akiwa kazini ni tishio kwa uhuru wa habari. Uhuru wa habari ni kumwezesha waandishi kufanyakazi bila vitisho ama ghasia na waweze kuripoti wakiwa huru bila kudhibitiwa. Kama mwandishi, Daudi Mwangosi alikuwa akitimiza haki yake ya kikatiba kufanya “kazi nzuri”. 

Kwa vyombo vya habari na hasa waandishi, haijalishi kama Kamanda wa Mkoa wa Polisi ameipiga marufuku shughuli za Chadema katika kijiji cha Nyalolo au la. Ilikuwa ni jambo ka maslahi ya umma kwa vyombo vya habari ambalo vyombo vya habari vilistahili kuripoti kadri mambo yalivyokuwa yaakiendelea na watu wenyewe kufanya uamuzi. Kimsingi, wakati wote na katika matukio yote, mazuri ama mabaya, waandishi lazima wawepo na wachukuliwe kama watu wasio na upande wowte.

 Pia, Polisi walitumia nguvu ya ziada bila sababu dhidi ya watu wasio na silaha katika kijiji cha Nyololo village.Katika hatua ya mwisho, ikawa vita ya polisi dhidi ya waandishi wa habari na hatimaye kuuawa kwa Daudi Mwangosi. Timu ya uchunguzi haikubali kabisa suala la kukosea utambulisho wa mtu. Waandishi wanane waliokuwep katika kijiji cha Nyololo waliweza kutambulika kwa urahisi, hasa kutokana na mambo kwenda salama katika eneo la uslamaa [A]. Waandishi walikuwa na Kamera, vidaftari na kalamu na wengine kama sio wote walikuwa wanafahamika sana na polisi wa Iringa. 

 Sasa imebainika wazi kwamba Polisi walikuwa wanawawinda waandishi wa Iringa ambao walikuwa wakiwajua. Mapambano ya Chadema na Polisi katika Kijiji cha Nyololo habari zake zilikusanywa na waandishi kutoka Dar es Salaam pia. Kwanini walikuwa waandishi wa Iringa ndiyo walilengwa katika ghasia hizo.! 

 Uhasama na chuki iliyokuwepo kati ya RPC wa Iringa na marehemu Daudi Mwangosi katika kipindi chote cha saa kadhaa tangu mkutano wa waandishi wa habaria na dakika chache kabla ya mauaji yake mbele ya RPC huyo huyo katika kijiji cha Nyololo Septemba 2, 2012 unaibua maswali mengi kuliko majibu. 

Waandishi sita wa Iringa wameathirika na msongo wa mawazo kutokana na kiwango cha ghasia walizofanyiwa na polisi na wanafikiria kuachana na kazi ya uandishi. Mmoja anapanga kuwa mchungaji kwa kuhofia maisha yake. Mamlaka husika zahitaji kuwa na mipango ya kuwaelimisha polisi jinsi ya kushughulika na vyombo vya habari hasa na wandishi wa habari. Lengo liwe kuboresha mahusiano ya kikao kati ya pande hizo mbili.. Hii inatokana na uhusiano mbaya iliyoibuka kati ya waandishi wa Iringa na polisi wa mkoa tgangu robo ya mwisho wa 2011. 

Uhusiano huu kati ya pande hizi mbili umekua tangu 2011 ambapo aliyekuwa OCD wa Iringa Mohamed Semunyu alipoamriwa ana bosi wake kulipa kamera ya mwandishi aliyoiharibu bila sababu ya maana. Inashinda ufahamu wa kawaida kwamba matukio mawili ya yanayofanana katika siku moja ynashughulikiwa tofauti.: Moja linashughulikiwa na ukatili na nguvu kubwa kwa kuwalenga wanahabari wa Iringa. 

Katika tukio la kwanza, RCO aliamua Chadema wanaweza kuendelea na masuala yao ya ndani katika ofisi yao na katika tukio la pili Mkuu wa polisi wa mkoa anaamua shughuli hizo zisimamishwe kwa vyovyote na hata kwa nguvu. Akigusia kwa kiasi mpambano wa Nyololo kati ya Polisi na wafuasi wa Chadema, Rais Jakaya Kikwete katika hotuba yake ya kila mwezi kwa taifa kwa mwezi wa September 2012, alisisitiza polisi kuepuka matumizi ya nguvu za kupita kiasi na kuwakumbusha watanzania na wanasiasa kuheshimu sheria za nchi na kuiona polisi kama wasimamizi wa amani na usalama. 

 Rais alifafanua kuwa Jeshi la Polisi lina mamlaka ya kuruhusu au kuzuia haki ya kufanya mikutano na maandamano ya vyama vya siasa. Taarifa za awali za maofisa wa ngazi za juu kuhusu mauaji ya M wangosi zilitofautiana na mtu anapoziangalia kutokana na ushahidi uliopatikana ni dhahiri kulikuwa na jitihada za kuficha ukweli. Tukio hilo limeharibu sifa ya Tanzania kimataifa kama nchi ya amani na ya demokrasia. Mauaji ya Mwangosi yalitokea wakati wa kufanyika mkutano wa Chama cha Umoja wa Mabaraza ya Habari Duniani (WAPC) ambapo MCT ilikuwa mwenyeji wake.

 Katibu Mkuu wa WAPC, Chris Conybeare, alimwambia waziri wa Habari, Dk. Fenella Mukangara: “Wakati waandisi wanauawa demokrasi pia inakufa.. tukio hili moja limeanza kuichafua sifa yaTanzania ya kuendeleza uhuru wa habari”. Zaidi ya Polisi saba chini ya uongozi wa RPC Michael Kamuhanda kwa pamoja wamemzingira na kumpiga Daudi Mwangosi. 

Kwanini wengine hawajashitakiwa, si suala linalohitaji uelewa wa kawaida. Hata hivyo uchunguzi hauwezi kuthibitisha kama mauaji hayo ya Mwangosi yalipangwa.