Tatizo la uhaba wa vyanzo vya maji katika maisha ya kila siku kwa Watanzania ni mzigo usiobebeka kwani ukiachilia vijijini hata mijini ni kero tupu.!Kwa vijijini ni kama picha inavyojionyesha, mwananchi huyu alikutwa akisota na kuhangaika kutafuta maji safi na salama kwa matumizi ya kawaida ya kila siku.Hata hivyo anaonekana kushindwa kuchota maji hayo ya dimbwi baada ya kutoridhishwa nayo kiafya.