Zaidi ya watu 1,000 waliuawa katika ghasia za baada ya uchaguzi Mkuu mwaka 2007 na kuna wasiwasi na hofu kuhusu vitendo vibaya zaidi vya kutia hofu huku Kenya ikielekea kwenye Uchaguzi Mkuu kwa mara nyingine mwezi Machi 2013.
Miaka minne baada ya mzozo mbaya zaidi kuhusu uchaguzi kuwahi kutokea tangu Kenya kujipatia uhuru mwaka 1963, taharuki imetanda kabla ya Uchaguzi Mkuu.Matukio haya ni onyo kuwa nchi hiyo isitumbukie tena katika ghasia zilizoshuhudiwa mwaka 2007 .Kwa sasa Ghasia kadhaa zilishuhudiwa katika eneo la Tana Delta ambako zaidi ya watu 100 waliuawa mwezi Agosti mwaka huu, wakati wa mapigano kati ya jamii za Pokomo ambao sana sana ni wakulima na Orma ambao ni wafugaji .
Chanzo cha ghasia kilikuwa ni rasilimali za maji na ardhi.
Mnamo mwezi Septemba mwaka huu mauaji ya Mhubiri wa Kiisilamu Mjini Mombasa,yalifuatiwa na ghasia na makabiliano makali kati ya polisi na waandamanaji mjini humo.
Tangu hapo, naibu waziri Mambo ya ndani Kenya, Mhe.Ferdinand Waititu alifikishwa Mahakamani kwa kosa la matamshi ya chuki na kuchochea ghasia mjini Nairobi.Ghasia zaidi zimeripotiwa Pwani mwa Kenya na katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa nchi.Ghasia hizi zimesababisha wasiwasi na hofu huku kinyang'anyiro cha uchaguzi kikishika kasi kabla ya uchaguzi wenyewe utakaofanyika mwezi Machi mwaka 2013.
Mauaji hayo huenda yakafungua ukurasa wa uchaguzi mpya wenye ghasia.
Ghasia za 2007 zilikuwa mbaya sana kiasi kwamba aliyekuwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan alilazimika kuingilia kati kushawishi pande zote kwenye mzozo huo, vyama vya ODM na PNU vya Waziri Mkuu Raila Odinga na Rais Mwai Kibaki kufanya mazungumzo na kusitisha ghasia kisha kuunda Serikali ya umoja wa Kitaifa.Serikali hiyo ya Umoja wa Kitaifa imefanikisha kuundwa kwa katiba mpya baada ya kura ya maoni kuhusu katiba mpya kupata kura ya ndio na kushinda. Wakenya wengi walitaka utawala wa majimbo na kuwepo sheria kuhusu haki za watu.
Lakini kabla ya juhudi za kuunda jopo maalum kusikiliza kesi za washukiwa wa ghasia za baada ya uchaguzi zilizuiwa na wanasiasa, hasa wale waliohusishwa na ghasia za baada ya uchaguzi .
Pia kulikua na juhudi za kuleta mageuzi kuhusu sera ya ardhi, mageuzi katika idara ya polisi, na sheria ya uongozi bora.
Mabadiliko mengine ambayo yalihitajiwa kufanywa hasa baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata yamepuuzwa.
Mdahalo mkubwa sasa ni kuhusu wanasiasa wawili ambao wanasubiri kufika tena mbele ya ,Mahakama ya ICC wiki chache tu baada ya uchaguzi wa mwezi machi mwaka ujao, kwa tuhuma za kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi mkuu 2007 ,ambao ni Waziri wa zamani wa fedha Uhuru Kenyatta na William Ruto, mwanasiasa machachar.,Hata hivyo wote wawili wanakana kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi na wanagombea urais.Mojawapo ya maeneo yaliyoathirika kutokana na ghasia ni Kibera eneo bunge la waziri mkuu Raila Odinga
Wakati huo, wanasiasa wanaendelea kujilimbikizia mishahara minono wakati wafanyakazi wa sekta ya umma wakilazimika kugoma wakidai mishahara na mazingira bora ya kazi.Ukweli ni kwamba maelfu ya wale waliopoteza makao yao kufuatia ghasia za baada a uchaguzi, bado wako katika kambi za muda hadi leo !.
Ifikapo mwezi Machi, Wakenya watapiga kura za magavana na maseneta kwa mara ya kwanza. Ushindani utakuwa mkali katika nyadhifa za utawala wa mikoa.
Hata hivyo hatima ya Kenya iko mikononi mwa Wakenya wenyewe.
Kila la heri kenya.
MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI KENYA.