Askofu mpya wa kanisa la Kianglikana kutawazwa
Askofu wa Durham, Justin Welby, ambaye pia ni mfanyakazi wa zamani katika sekta ya mafuta, anatarajiwa kutajwa kama askofu mpya wa Canterbury.
Inaaminiwa kuwa askofu huyo, mwenye umri wa miaka 56, atateuiliwa kuchukua nafasi ya askofu Rowan Williams, atakayeachia ngazi mwezi Disemba baada ya miaka kumi uongozini.Habari zaidi kutoka makao makuu ya waziri mkuu nchini humo, zinasema kuwa askofu huyo atatangazwa rasmi siku ya Ijumaa.Askofu Welby, aliteuliwa kama askofu mwaka mmoja uliopita alipochukua wadhifa wa nne kwa ukubwa katika kanisa la kianglikana nchini Uingereza.
Mnamo Jumanne, wadadisi waliwacha kubahatisha kuhusu nani atachukua wadhifa huo baada ya watu wengi kutabiri kuwa yeye ndiye atachukua nafasi ya Rowan Williams
Jarida la Daily Telegraph, lilinukuu kuwa Askofu Welby amekubali kuchukua wadhifa huo ingawa kwa sasa hangeweza kutoa tamko lolote kuhusu udadisi juu yake.
Askofu Welby alisomea chuo kikuu cha Cambridge na kisha kufanya kazi katika sekta ya mafuta kwa miaka kumi na moja kabla ya kusomea dini ambapo baadaye alitawazwa mwaka 1992.