Rais Hu Jintao kwenye kongamano la kuwachagua viongozi wa chama cha kikomunisti
Hata hivyo Rais Hu Jintao ametoa onyo kali kwa wafisadi wa nchi hiyo akisema kuwa ufisadi bado unaendelea kuwa tatizo kubwa nchini humo Aidha Rais Hu anatazamiwa kujiuzulu kutoka wadhfa wake wa uongozi wa chama na kumkabidhi Xi Jinping anayeonekana kuwa kiongozi wa siku za usoni wa Uchina.Akihutubia zaidi ya wajumbe 2,000 mjini Beijing, Rais Hu Jintao alisema kuwa kukosa kushughulikia tatizo hilo, huenda kukasababisha pigo kubwa kwa chama.
China ilipata mafanikio makubwa katika kipindi kilichopita ingawa changamaoto nazo zilikuwa nyingi.
Alitoa wito wa kuwepo malengo makubwa pamoja na kuhimiza bidii.
Hotuba yake ilifungua rasmi mkutano wa wiki moja utakaoshuhudia kuteuliwa kwa viongozi wapya wa chama.
Hali ya usalama imedhibitiwa mjini Beijing, huku wanaharakati wakiwa wamezuiliwa au kupewa kifungo cha nyumbani, kulingana na mashirika ya kibinadamu.
Viongozi wazee watastaafishwa
Bwana Hu aliwaaambia wajumbe kuwa lazima nchi hiyo ifuate nyayo za dunia ambayo inabadilika kila kukicha pamoja na kuzingatia mabadiliko katika mazingira ya nyumbani.
''Lazima tuwe na malengo makubwa, tufanye kazi kwa bidii na tuendeleze maendeleo ya kisayansi, tuimarishe ushurikiano na pia maisha ya watu wetu.'' alisema bwana Hu
Mageuzi yatakayofanywa:
Mkutano maalum wa chama cha kikomunsiti kufanyika kila baada ya mwongo mmoja
Viongozi wenye zaidi ya miaka 68 watasataafishwa
Viongozi wapya wakuu kutajwa.
Viongozi hao wameamuliwa lakini bado hawajatajwa.
Mirengo ni muhimu kuliko sera na mfumo wa uteuzi haueueleweki