November 13, 2012


Balozi wa kinywaji cha Hennessy awasili nchini na kutambulisha rasmi vinywaji vya kampuni ya 
Q Way International & CO.
Balozi wa kinywaji cha Hennessy, Cyrille Gautier Auriol akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu utumiaji wa vinywaji vya kampuni hiyo katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Ziara hii ya balozi Auriol ni ya pili hapa nchini ndani ya miezi 12.
Hennessy ni kinywaji kinachopendwa sana duniani ikiwa inatengenezwa Ufaransa ambapo tangu kutambulishwa kwake hapa nchini kinywaji hiki kimepata soko kubwa tene kwa muda mfupi na kuacha watumiaji wake waongezeke siku hadi siku jambo ambalo Balozi huyo alilisifia na kuwaomba watumiaji wa kinywaji kusaidia kutambulisha uzuri na sifa za kinywaji hiki. 

 Balozi Cyrile G. Auriol kushoto akiwa na timu yake ya mauzo nchini Tanzania. Katikati ni meneja mauzo wa kampuni(Q Way International) ndugu Omary na ndugu Hassan Ali ambaye ni mchanganyaji - mixologist wa kampuni hiyo

 Afisa masoko wa Q Way International ndg,Omary  akiongea na waandishi wa habari

Pia balozi wa kinywaji cha Hennessy, Cyrile Gautier Auriol, amewasili nchini kwa dhumuni la kuelimisha na kujenga uelewa kuhusu utumiaji wa vinywaji vya kampuni hiyo katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Balozi huyo ambaye atakua nchini kwa muda wa siku mbili ikiwa ni katika ziara yake ya siku  katika ukanda wa Afrika Mashariki pia atatoa mafunzo hayo kwa wahudumu mbalimbali wa bar kubwa mbalimbali hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa elimu hiyo itatolewa nchi zote za Afrika Mashariki kwa lengo la kuwapa elimu juu ya uchanganyaji wa kinywaji hicho ili kuwaongezea uelewa katika ufanyaji wao wa kazi za kila siku.

Ameongeza kuwa baada ya ziara hiyo ataendelea kufanya ziara katika nchi zingine za ukanda huo kwa lengo la kuzidi kuhamasisha matumizi ya kinywaji hicho.

Ziara hiyo itahitimishwa na kuwaelimisha na kuwaburudisha wageni maalum wakiwemo wanamitindo maarufu na wafanyabiashara na pia atazindua chumba cha kinywaji hicho katika Club 327.

'Kutakua na kikao maalum na wapenzi wakubwa wa kinywaji hicho na kuwazawadia mialiko ya kuingia kwenye klabu ya wapenzi wa kinywaji hicho Afrika Mashariki' amesema balozi huyo.