Baraza la mawaziri nchini Kenya linapendekeza mabadiliko makubwa kwa sheria za ndoa nchini humo .
Mswaada wawaliowasilisha unapendekeza kuwa wanaume wanweza kuoa zaidi ya mke mmoja na hata kuharamisha mahari ambapo familia ya mwanaume inalipa mahari hiyo. Mapendekezo hayo tayari yamezua hisia kali kutoka kwa jamii kwa ujumla. Aidha mswaada huo, lazima uidhinishwe na bunge kabla ya kufanywa sheria.Pia inataka kuhalalisha watu kuishi pamoja kama mume na mke bila ya ndoa kwa kipindi cha miezi sita kama njia ya kulinda watoto na wanwake wakati uhusiano huo unapovunjika.
Wengi wa wanaoishi maisha kama hayo ni wanafunzi wa vyuo vikuu ambapo uhusianao kama huo unajulikana kama "come we stay" au njoo tuishi pamoja kama mke na mume bila ya ndoa.
Wanafunzi hujipata katika uhusiano kama huo kwa hata miaka minne au zaidi wakati wakisoma na punde baada ya kuhitimu , huvunja uhusiano ule.
Mara nyingi watu huishi pamoja bila ya kuoana kwa sababu za manufaa ya ule uhusiano
Wakati mwingine hata hupata watoto wakati wa kipindi kile wanapoishi pamoja , na hapo ndipo mwanamue hutafuta njia za kutoroka ili kukwepa majukumu yake.
Na hilo ndilo lengo la mswaada huu kulingana na baraza la mawaziri.
Linasema linataka ikiwa utakuwa sheria iweze kulinda akina mama na watoto kutokana na dhulma za nyumbani hususan wanaume wanaokwepa majukumu yao.
Mswaada huu umevutia hisia mbali mbali, baadhi wakisema kuwa itakwenda kinyume na tamaduni na desturi za jamii, hasa ikizingatiwa swala la mahari ambalo mswaada huo unapendekeza kutupiliwa mbali.
Dini nyingi kama Uisilamu na hata wahindi wanakumbatia swala na mahari kwa sababu ni matakwa ya dini.
Ingawa baraza la mawaziri limepitisha mswaada huo, inaweza tu kuwa sheria ikiwa bunge litaipitisha. Ikiwa kweli rekodi ya bunge hili ndio itakuwa kigezo cha kupitishwa kwa mswaada huu, bunge lenyewe lenye asilimia hamsini ya wanaume, litatupilia mbali mswaada huo au kuupitisha baada kufanya mabadiliko.
Wengi wa wanaoishi maisha kama hayo ni wanafunzi wa vyuo vikuu ambapo uhusiano kama huo unajulikana kama "come we stay" au njoo tuishi pamoja kama mke na mume bila ya ndoa.
Wanafunzi huishi katika uhusiano kama huo kwa hata miaka minne au zaidi wakati wakisoma na baada ya kusoma huachana.
Mara nyingi watu huishi pamoja bila ya kuoana kwa sababu za kujinufaisha kwa hali yoyote ile.
Wakati mwingine hata hupata watoto wakati wa kipindi kile wanapoishi pamoja , na hapo ndipo mwanamume hutafuta njia za kutoroka ili kukwepa majukumu yake.
Mswaada huu umvutia hisia mbali mbali, baadhi wakisema kuwa itakwenda kinyume na tamaduni na desturi za jamii, hasa ikizingatiwa swala la mahari ambalo mswaada huo unapendekeza kutupiliwa mbali.