November 09, 2012


Mali yazidi kutumbukia katika mzozo wa kibinadamu.

Mkuu ya kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu  ICRC anasema hali ya kisiasa na ukosefu wa uthabiti wa kijeshi nchini Mali inazidi kuiingiza nchi katika mzozo wa kibinadamu. Anasema ana wasi wasi kwamba mtizamo mdogo unatolewa kwa hali ya kibinadamu nchini Mali na wanasiasa wa kimataifa na wakubwa wa kijeshi.Mali si mgeni wa mizozo ya kibinadamu.  Kwa wakati huu inakabiliwa na mzozo wa muda mrefu wa chakula, ambao rais wa kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu, Peter Maurer anasema umechanganyika na kuvunjika kwa mfumo wa kisiasa.

Hali ni mbaya zaidi upande wa kaskazini, ambako makundi ya kiislamu yenye msimamo mkali yamewang’oa wanajeshi na waasi wa tuareg ambao kwa muda mrefu wamekuwa katika mapigano kudai taifa huru upande huo.
Waislamu wenye msimamo mkali wanajitenga na jamii ya watu wa huko na kuwatisha watu. Pia wameleta matatizo makubwa kwa mashirika ya misaada yanayojaribu kufanya shughuli zake katika eneo hilo.
Maurer anasema ICRC imekuwa ikifanya kazi kwa miezi kadhaa kuboresha fursa ya kuwafikia watu wenye shida upande wa kaskazini.
Anasema idara yake hivi sasa inagawa chakula kwa takriban watu laki nne na elfu 20. Ukiongezea hilo, anasema ICRC inagawa madawa na vifaa vingine kwa mahospitali katika mji wa gao na vituo vya afya katika maeneo hayo.
 Lakini anasema ana wasi wasi kwamba wanasiasa na watunga sera wa kijeshi huenda hawatilii maanani sana hali ya kibinadamu ya mali katika mazungumzo yao.  Anasema hili lilikuwa suala la kufuatiliwa na maafisa waandamizi wa serikali ambao alikutana nao katika ziara yake nchini Niger na Mali mwishoni mwa October.