November 13, 2012


Maandamano kupinga ufisadi Uganda

Ramani ya Uganda
Polisi nchini Uganda wamewazuia wanaharakati wa kupinga ufisadi kufanya maandano katika barabara za mji mkuu wa nchi hiyo, Kampala.
Karibu wanaharakati 300 waliokuwa wamevalia nguo nyeusi walilazimika kukatiza maandamano yao baada ya polisi waliojihami kwa silaha kuziba barabara zote.
Mwanahabari wa BBC amesema maandamano hayo yamefanyika kufuatia ufichuliwai katika vyombo vya habari kuhusu tetesi  kadhaa za ufisadi ikiwemo kwamba zaidi ya dola milioni 15 za misaada ya kigeni zimeishia mifukoni mwa wakuu fulani serikalini.