November 13, 2012

Bunge nchini Somalia limeidhinisha baraza jipya la mawaziri kumi waliloteuliwa na waziri mkuu Abdi Farah Shirdon. Wanawake wawili ni miongoni mwa walioteuliwa.
Wabunge wa SomaliaSerikali kwa mara ya kwanza ina waziri wa kwanza mwanamke atakayeshikilia wadhifa wa waziri wa mambo ya nje, Fauzia Yusuf Haji Adan na ambaye anatoka Somaliland.
"Wabunge walipitisha baraza hilo kwa kura 219 , kati ya wabunge 225, waliohuduhuria kikao'' alisema spika wa bunge Mohamed Osman Jawari.Kuidhinishwa kwa baraza hilo kumekuja licha ya ripoti kuwa baadhi ya koo hazikuwakilishwa vyema kwenye baraza hilo liliotajwa wiki moja iliyopita.
Wabunge watatu waliwakataa mawaziri hao huku wengine watatu wakijizuia kupiga kura.''
Rais mpya pamoja na wabunge wapya walichaguliwa hivi karibuni nchini Somalia , nchi iliyokuwa haina serikali thabiti kwa zaidi ya miaka 20.
Serikali mpya inakabiliwa na changamoto nyingi wakati ikijaribu kuleta utulivu na utahbiti katika nchi hiyo ambayo imekumbwa na vita vya muda mrefu pamoja na tisho la wanamgambo wa Al Shabaab ambao wametishia kuipindua wakisema inaungwa mkono na nchi za Magharibi.