Mauzo ya tiketi ya fastjet yazinduliwa Tanzania.
Nauli za chini zaidi kuwahi kutokea zatajwa, watanzania wengi zaidi wataweza kupanda ndege kwa safari zao hapa Tanzania na baadae Afrika.
Ndg Richard Bodin pichani kushoto [Afisa Biashara Mkuu wa Shirika la Ndege la Fastjet ] ,akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu uzinduzi wa mauzo ya tiketi za shirika hilo hapa nchini. SHIRIKA la Ndege la kwanza Afrika la nauli nafuu fastjet, leo limezindua mauzo ya tiketi zake nchini Tanzania, ikiwa ni maandalizi ya safari yake ya kwanza ya kibiashara mwishoni mwa mwezi huu.Uzinduzi wa tiketi hizo ni hatua muhimu katika juhudi za kampuni hiyo kuwezesha usafiri wa ndege kwa watanzania, wako wengi ambao awali walikuwa hawamudu gharama za safari za ndege.
Huku nauli za anga zikiwa zinaanzia Tsh32,000 (USD20) kabla ya kodi za serikali (VAT), usafiri wa anga sasa unakuwa moja ya njia nafuu za watu kusafiri.
Fastjet ambayo imeinunua FLY540, imechagua Dar es Salaam kuwa kituo chake cha kwanza cha uendeshaji Barani Afrika, huku safari za ndege zikiwa zimepangwa kuanza kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Juluis Nyerere kuanzia Novemba 29.
Tiketi za Dar es Salaam-Kilimanjaro na Dar-Mwanza zinaanza kuuzwa kuanzia leo. Safari zingine za ndani na Kanda ya Mashariki mwa Afrika, zitaanza baada ya wiki kadhaa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa fastjet, Ed Winters amesema kuwa "Hiki ni kipindi cha kihistoria kwa safari za anga Tanzania na hasa Afrika. Usafiri wa anga siyo tena himaya ya watu wachache Tanzania. Fastjet itafanya usafiri wa anga kuwa kitu ambacho watanzania wengi wanakimudu tofauti na awali, hivyo kutoa fursa nzuri kwa zaodo kwa wafanyabiashara, safari za likizo na wanafamilia kutembeleana".
Tiketi zinapatikana kupitia mawakala wa usafiri wa na dawati la mauzo, kituo cha mawasiliano na ofisi za fastjet yenyewe. Tovuti mpya ya fastjet, www.fasthet.com itazinduliwa wiju ijayo na kutoa taarufa za safari na nauli. Tovuti hiyo pia itaruhusu kununua tiketi kwa kutumia kadi za credit/debit pamoja na simu za mkononi.