Rais wa Marekani Barack Obama ametembelea baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa vibaya na kimbunga huko kwenye pwani New Jersey,akiwaambia wakazi walioathirika vibaya kwamba serikali kuu itawasaidia kwa kuwawezesha kutokana na maafa hayo.
Akisindikizwa na Gavana wa jimbo hilo Chris Christie Bw.Obama aliwahakikishia mamilioni ya wakazi wa New Jersey na wakazi wengi wa jiji kuu la New York . Alitoa rambi rambi kwa kwa familia zilizopoteza ndugu na wapendwa wao na kuahidi “tutafuatilia mpate kila msaada mnaohitaji ili kujijenga upya”.
Rais pia alisema makampuni ya umeme yaliyo mbali na eneo hilo mpaka huko Carlifornia yameahidi kusaidia. Alisema ameagiza ndege za kijeshi kusafirisha vifaa na wafanyakazi kuelekea eneo hilo haraka iwezekanavyo.