Pengo kati ya maskini na matajiri lapanuka
Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la Save the Children linaonya kuwa pengo kati ya watu maskini na matajiri limekuwa kubwa sana katika miaka ya hivi karibuni na kuwa kubwa hali ambayo siyo nzuri kwa mfumo wa maisha ya kawaida.!
Shirika hilo linasema kuwa pengo hilo limekuwa kubwa na linawaathiri zaidi watoto.
Kwa mujibu wa Save the Children, linasema kuwa hali ya vifo vya watoto wachanga imepungua ingawa katika sehemu zingine bado kuna changamoto.
Ripoti yenyewe ambayo inakuja kabla ya mkutano mkuu wa umoaj wa amatifa kuhusu umaskini, inasema kuwa huenda hatua za hali kuimarika zikaathirika ikiwa hali hiyo haitashughulikiwa vyema.