TAMKO LA ASKOFU METHOD KILAINI DHIDI YA GAZETI LA MWANANCHI LEO 16 NOV
Askofu Method Kilaini
TAMKO – STATEMENT
Kwa masikitiko makubwa nimesoma katika gazeti la Mwananchi kwamba nimeiponda safu ya uongozi na sekretarieti ya CCM. Mimi sijaongea na gazeti lolote juu ya uongozi wa CCM na wala sina nia au sababu ya kuuponda uongozi huo. Ni vibaya kwa gazeti lolote lile kutumia jina la mtu kwa kueneza maoni yake. Kama ni waugwana natumaini watasahihisha waliyoyaandika. Nasikitika sana kwa kunikwaza na hilo.
Askofu Kilaini
Askofu Method Kilaini
Bukoba Catholic Diocese
e-mail: mkilaini@gmail.com
http://card-rugambwa.catholicweb.com