November 16, 2012


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa Mhadhara wa 13 wa Kumbukumbu ya Hayati Moringe Sokoine, uliofanyika leo, kwenye Ukumbi wa 'Nelson Mandera Freedom Square' Kampasi ya Solomon Mahlangu, katika Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) mjini Morogoro.
 
Sehemu ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha SUA wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akitoa mhadhara wa 13 wa kumbukumbu ya Hayati Moringe Sokoine, uliofanyika leo, kwenye Ukumbi wa 'Nelson Mandera Freedom Square' Kampasi ya Solomon Mahlangu, katika Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) mjini Morogoro.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha SUA, Alnoor Kassim, baada ya Makamu kutoa   mhadhara wa 13 wa kumbukumbu ya Hayati Moringe Sokoine, uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa 'Nelson Mandera Freedom Square' Kampasi ya Solomon Mahlangu, katika Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) mjini Morogoro, leo.