Uingereza yatoa ilani ya ugaidi Misri
Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Uingereza imeonya kuwa kuna uwezekano wa kutokea mashambulio ya kigaidi katika eneo la Sinai nchini Misri, na imelipa uzito wa juu onyo hilo kutokana na hofu ya mashambulio hayo kuwa kubwa zaidi.
Tahadhali hiyo inatolewa kutokana na taarifa za hivi karibuni kuhusu shukio la njama za al-Qaeda na kupatikana kwa silaha katika eneo la Sinai Misri.
Ikumbukwe hivi karibuni polisi nchini Misri waligundua kundi la kigaidi Jijini Cairo, na baadhi ya taarifa zinaeleza magaidi hao wlikuwa wakipanga kushambulia watalii kutoka mataifa ya Magharibi.
Hata hivyo Wizara ya Mashauri ya Nchi za Nje ya Uingereza inasema hali katika maeneo ya watalii ya Bahari ya Sham, pamoja na Sharm el Sheikh, ni tulivu kwa sasa.