Umoja wa Mataifa unahimiza kupima mapema saratani ili kupunguza vifo
Siku ya kimataifa ya Saratani huadhinishwa kote ulimmwenguni kila Februari tarehe 4, ambapo kauli mbiyu ya mwaka 2012 ni “Together it is Possible” – yaani "Kwa pamoja Inawezekana".
Shirika la Afya Duniani WHO, limeeleza kwamba kupimwa watu mapema ndio njia pekee ya kupunguza vifo milioni 8 vinavyotokea kutokana na ugonjwa wa saratani kila mwaka kote duniani.WHO inasisitiza umuhimu wa kuwepo na mpango wa kuwapima watu wote wenye afya nzuri ili kuweza kugundua ugonjwa huo wa hatari mapema na kwa urahisi zaidi. Ikiadhimisha siku ya saratani Umoja wa mataifa unakunbusha dunia kwamba ugonjwa huo unasababisha asili mia 13 ya vifo vyote duniani.Mwandishi wa Sauti ya Amerika mjini Mombasa Josephat Kioko anaripoti kwamba ugonja huo ambao zamani ulichukuliwa kama ugonjwa usojulikana na kuwapata watu matajiri, unazidi kuwa umizi wananchi maskini kutokana na gharama kubwa za matibabu
.