November 03, 2012

Bashir na Kiir waendelea na mashauriano

Marais wa Sudan na Sudan Kusini wanakutana kwa siku ya pili leo Jumatatu wakijaribu kufikia makubaliano kuhusu masuala ya muda mrefu ambayo hayajasuluhishwa tangu nchi hizo mbili zigawanyike mwaka jana.

Mazungumzo kati ya Rais Omar al Bashir wa Sudan na Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini yameendelea leo katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Msemaji wa Sudan amesema baada ya duru ya awali ya mashauriano siku ya Jumapili pande hizo mbili zimekubaliano katika masuala mengi  kama uchumi, mafuta na biashara, lakini bado wamegawanyika katika masuala ya usalama.
Mizozo imetokea pale Sudan Kusini ilipojitangazia uhuru wake July 2011  kutoka Sudan na kusababisha kutokea kwa mzozo kuhusu mkoa wa Abyei wenye utajiri wa mafuta.
Sudan pia inaishutumu kusini kwa kuwapatia silaha waasi katika mikoa miwili ya kusini, wakati Sudan Kusini inalishutumu jeshi la Sudan kwa upigaji mabomu.
Umoja wa Mataifa umezipa pande nchi hizo mbili mpaka Jumamosi kufikia muafaka au zitakabiliwa na vikwazo