November 17, 2012

UKATILI KWA WATOTO

MTOTO ALIYEUNGUZWA MKONO NA KULISHWA KINYESI AKATWA MKONO HOSPITALI YA RUFAA YA MBEYA

Mtoto Aneth Johanes miaka minne baada ya kuchomwa moto na mama yake mdogo Bi Wilvina Mkandala (miaka 24)baada ya kumfungia ndani na kumchoma kwa maji ya moto.!
Siku Mtoto Aneth Johanes akiwa amepumzika kwa matibabu katika Hospitali ya Rufaaa Mbeya baada ya kukatwa mkono wake wa kushoto na sasa kuanza kuishi maisha mapya ya ulemavu wa kiungo.
Mtoto Aneth Johanes akiwa anaendelea vizuri kwa matibabu na kupata faraja kwa kumuona mama yake mzazi aliyefunga safari kutoka Mkoani Kagera na kuja kumuuguza mwanae








Pichani kushoto:
Mama mzazi wa Mtotot Aneth akiwa kagubikwa na mawazo baada ya kufika hospitalini kumfariji mwanae anayeendelea kupata matibabu baada ya kukatwa mkono wake.
Hakika inauma sana..





Hata hivyo Mwanamke anayetuhumiwa kumnyanyasa mtoto wa dada yake kwa kumfungia ndani na kumchoma kwa maji ya moto, hatimaye amepandishwa kizimbani leo katika mahakama ya Wilaya ya Mbeya kujibu shtaka linalomkabili.

Mwendesha mashtaka wa Serikali, Achiles Mulisa ameiambia Mahakama kuwa Mtuhumiwa Wilvina Mkandala (24) alitenda kosa la kusababisha majeraha akiwa na nia ovu ambayo imemsababishia ulemavu mtoto  Aneth.
Mulisa akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo Gilbert Ndeuruo amesema kosa hilo ni kinyume cha kanuni ya adhabu kifungu  cha 222(a) sura ya 16 kama ilivyorejewa mwaka 2002.
Kutokana na kosa hilo mshtakiwa amekana shitaka hilo ambapo amerudishwa mahabusu hadi Novemba 22, Mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Mwendesha mashtaka huyo alisema Mshakiwa amenyimwa dhamana kutokana na hali ya mhanga ambaye ni mtoto Aneth kutokuwa ya kuridhisha na kuongeza kuwa sababu nyingine ni kwa ajili ya usalama wake.
Alisema upande wa Jamhuri unamashahidi wanne ambao wataanza kutoa ushahidi wake mahakamani hapo Novemba 22, Mwaka huu kutokana na upelezi kukamilika.
Aliwataja mashahidi hao kuwa ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Shukuru Mwakanyamale, Daktari anayemtibu mhanga katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya Dr. Paul.
Wengine ni Askari Polisi aliyepeleleza kesi hiyo WP Pudensia na Habiba Mwakanyamale ambao wako tayari kufika mahakamani na kutoa ushahidi wao mbele ya mahakama.
Awali mshatakiwa huyo aliieleza mahakama kuwa na uhusiano na mtoto  huyo ambapo pia alikiri kuwa na taarifa za kile kinachoendelea juu ya matibabu ya mtoto huyo na kuhusu kukatwa kwa mkono wake wa kushoto na kufungwa bandeji ngumu(POP) kwenye mkono uliobaki.
Habari na: mbeyayetu blog