November 17, 2012

Kipigo cha kufa mtu. Nusura kuchomwa moto live !

Baada ya mabishano yasiyo na tija kwa mdai ghafla kipigo kikaanza kwani mabishano hayo tayari yalisogeza umati mkubwa wa watu ambao walihamaki na kuanza kumpa kipigo mdaiwa ili akome tabia ya kutapeli.
Mtuhumiwa akishikishwa adabu na kwa kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali

"Nitamlipa hela yake yote leo..nimekoma sirudii" mtuhumiwa alisikika akijitetea  kwa bidii.

Mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi baada ya kutuhumiwa kumtapeli rafiki yake wa ukweli kikazi, zaidi ya Tsh 245,000/= na kuamua kumzungusha kwa muda usioonesha nia ya kumlipa. Taili la gari pembeni tayari liliandaliwa ili kutumika kumchoma mtuhumiwa!!
Aliyetapeliwa akaamua kumnusuru mtuhumiwa wake asichomwe moto maana angekosa  anachodai
Bado aliendelea kukimbizwa.......!
Ni hatari